Tumain na mabutu yake kichwani akijiandaa kwenda kanisani.
.
Na Dustan Shekidele. Mogogoro.
HAPA Chini ya Juwa[Duniani] kuna vyeo vingi serikalini,Taasisi za dini na taasisi binafsi, Vyeo vyote hivyo vina ukomo mfano mtumishi akistaafu anavuliwa cheo hivyo anakabidhiwa bosi mwingine na huyo aliyetoka anabadilishwa jina anaitwa mstaafu.
Lakini Cheo cha kuitwa Baba au Mama ni cha kudumu hakina ukomo[ustaafua] na heshima yake ni ya kudumu haijalishi Mzazi ana kitu[Mali] au fukara[hana kitu].
Septemba 20 Majira ya Saa 11 na dakika 21 Jioni Wodi ya wazazi [Reba]hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro kwa mara ya kwanza Dustan shekidele alitunukiwa cheo cha kuitwa Baba.
Hii ni baada ya Tumain. Rehema Dustan Shekidele kuzaliwa siku na muda tajwa hapo juu Miaka kadhaa iliyopita.
Asante Sasa Mwenyezi Mungu kwa zawadi na heshima hiyo ya kuitwa baba Asante sana Mwamvua Mariam Shilla kwa kunizalia Mtoto na kunipa heshima ya kuitwa baba, Asante sana binti yangu Tumaini kwa kuniheshimisha kuwa wa kwanza kunipa cheo cha kuitwa baba, baadae wakafuata wadogo zako Hayati Shilla mwenzi Mungu ampunzishe kwa Aman,
Neema na Glory, shangaza zako, Baba zako wakubwa na wadogo, Mama zako wakubwa na wadogo wajomba zako, bibi zako ulio rithi majina yao Tumain bibi yako Mzaa baba na Rehema bibi yako Mzaa Mama kwa pamoja tunakutakia kheri ya kumbukizi yako ya siku ya kuzaliwa ‘Happy Birthday’.
Wosia wangu kwako Mwanangu ’First Born’endelea kushika mafundisho ya Mwenyezi Mungu na kuwatii wazazi wako sambasamba na ndugu, jamaa na marafiki hiyo itakuwa hadhina yako kubwa duniani na Mbinguni.
Kwa kufanya hivyo Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema atakuongezea umri zaidi wa kuishi kwani kupitia maandiko yake matakatifu amethibitisha hilo kwenye amri 10 za Mungu kwenye amri ya 4 nayo inasema hivi.
“Waheshimu baba na Mama upate miaka mingi na heri duniani”
.





No comments:
Post a Comment