Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, September 30, 2025

BARTHDAY YA NYOTA WA TAIFA STARS YAFANA,

Na Dustan Shekidele, Morogoro,

SHEREHE ya Kumbizi ya Siku ya kuzaliwa’Happy Birthday’ ya Mchezaji nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’imefana vilivyo baada ya walikwa kula na Kunywa Mwanzo Mwisho,

Nyota huyo si Mwingine ni Peter Tino aliyefunga bao pekee Jijini Ndola  Zambia Mwaka 1979 dhidi ya Timu ya Taifa ya Zambia ‘Kipolopo’

Bao hilo Pekee lililowanyamazisha Wazambia kwenye uwanja wao wa Nyumbani liliipa tiketi Tanzania ya kufudhu kwa mara ya kwanza  mashindano ya Mataifa ya Afrika yaliofanyika mwaka 1980  nchini Nigeria.

Peter Tino Mkazi wa Kigurunyembe Mkoani Morogoro jumapili iliyopita Septemba 28 alifanya sherehe yake ya kumbukizi ya kuzaliwa nyumbani kwa Mpwa wake Mtaa Maarufu wa Tubuyu B Kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro, lfahamike Mtaa huyo wa Tubuyu wanaishi Mastaa wengi akiwemo Mzee Ramadhan Kichuya baba mzazi wa Shiza Kichuya Staa mwingine ni anayeishi mtaa huo ni Emanuel Kimbawala katibu Mkuu wa zamani wa chama cha Soka Mkoa wa Morogoro,

Katika sherehe hiyo iliyoratibiwa kisomi kundi a wageni waalikwa wali ‘Enjoy’ kwenye vipengere vyote vitatu muhimu Kula,Kunywa na Kucheza.

Kabla ya kukata keki ukumbi mzima ulisimama na kumfanyia maombi Maalum ‘Streka’ huyo wa zamani wa timu ya Pan Afrikam ya Dar es salaam.

Baada ya maombia hayo Mshambuliaji huyo aligongewa muziki wa zamani na kulisakata Rhumba huku akimwagiwa bia kichwani ikiwa ni ishara ya kuadhimisha siku yake hiyo muhimu kwenye maisha yake.

Akizungumza na Mtandao huu  Tino alisema

” Leo nimetimiza Miaka 66 namshukuru sana mwenyezi Mungu kwa kunijaia kufika umri huu mkubwa kuna wengi walitamani kufika umri huu lakini ahawakufanikiwa”

Kipengele cha Mwisho kwenye sherehe waalikwa wakimshika Mkonono wa pongezi shujaa huyo wa Tanzania kwenye medani ya Soka Mtandao huu Unamuomba Mwenyezi Mungu azidi kumlinda shujaa wetu huyo aliyemwaga jasho lake uwanjani kuipigania nchi yake ya Tanzania,

Friday, September 26, 2025

HII NDIO MORO YA VIPAJI. WANA MOROGORO MTU NA MDOGO WAKE WANYAKUA UBINGWA WA MAGARI AFRIKA.

Picha no Ahmed na msomaramani wake Vill Oslaj kulia wakiwa juu ya gari huku wakishangalia.

Picha no 2.3 na 4 Shanto na mdogo wake wakikumbatiana kwa furaha baada ya kuibuka washindi.

Picha no 3 Shantona Weleed wakiwa na watoto zao

Picha no 4 Shanto na Waleed wakiwa na vikombe.

Picha no 5 Waleed wapambe wake akiwa juu ya gari lake lenye rangi nyekundu baada ya kuibuka mshindi.

        Na Dustan Shekidele,Morogoro.

WATU wanaposema Morogoro ni Mkoa wa Vipaji.hawatanii wanamaanisha ukweli mtupu,  kauli hiyo Imeendelea kuthibitishwa wiki iliyopita baada ya madereva wa magari wana Morogoro watatu kunyakua ubingwa wa mbio za magari Afrika.

Wana Morogoro hao walioshinda ni Ahmed Huwel kutoka kiwanda cha Tumbaku cha Mkwawa Morogoro aliyeshika nafasi ya kwanza na Shanto  Nahdy pia kutoka Mkwawa alinyakua nafasi ya pili huku Mdogo wake Waleed Nahdy akitwaa nafasi ya tatu.    

                 TUJIKUMBUSHE

Mwaka 2003 Mwana Morogoro Mwisho Mwampamba alishika nafasi ya pili ya Mashindano ya Big Brather Afrika ‘BBA’ ndani ya jumba la sanaa nchini Afrika Kusini,

Mwaka uliofuata 2004 Mwana Morogoro Seleman Msindi Afande Sele alinyakua Ubingwa wa Mfalme wa Rhymes Tanzania ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam.

 Kama hiyo aitoshi Bondia Francis Cheka alinyakua ubingwa wa Ngumi Tanzania baada ya kuwatwanga mabondia mbali mbali ikiwemo familia nzima ya masumbu ya Matumla,

Baada ya Cheka kuchuja kamuachia Grops Mdogo wake Cosmas Cheka ambaye naye aliuwasha Moto ule ule uliowashwa na kaka yake.

Baada ya familia hiyo ya Cheka Kupotea kwenye Ngumi kwa sasa wameibuka Mabondia wengine wana Morogoro  Twaha Kassim Maarufu Twaha Kidugu Mzee wa Bendera Chuma Mlingoti Chuma’Show Show’ na Karim Mandonga ‘Mtu kazi’  mzee wa Ngumi kirumbi rumbi,

Kwenye Soka sasa wana Morogoro wako wengi lakini kwa sasa niwataje wachake Dickson Job Kibwana Shomari Abuutwarib Msheri wote hao ni wachezaji tegemo wa Yanga,

Kwa upande wa Simba yupo Shomari Kapombe, Abdulrazake Spear Hamza na Mzamiru Yassim ambao pia ni tegeo la Simba,

Wana Morogoro wengine ni Aishi Manura,Pascal Msindo na Teps Evans wanaokipiga Azam Fc.

Kama kawaida Mtandao huu umekusanya habari kibao za chini ya kapeti hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote,

                       CAPTION

HII NDIO MORO YA VIPAJI.

WANA MOROGORO MTU NA MDOGO WAKE WANYAKUA UBINGWA WA MAGARI AFRIKA.

Thursday, September 25, 2025

MGANGA AIBUKA KIDEDEA MBIO ZA MAGARI AFRIKA

Mshindi  Lasin Nasser akionyesha kidole kmoja kama ishara ya kuwa mshindi wa kwanza Afrika

Na Dustan Shekidele,Morogoro.

RAIA wa Uganda Nasin Nasser ameibuka kidedea mashindano ya  Magari Afrika alofanyika wiki iliyopita Mkoani hapa.

Mashindano hayo yalioshirikisha madereva 23 kutoka nchi mbali mbali barani Afrika yalianza kutimua vumbi September 19 na kutamatika September 21 na mganda huo kuibuka mshindi wa kwanza.

Mara baada ya dereva huyo na msomaramani wake kukabidhi vikombe na Mgeni rasm Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe Mussa Kilakala.kundi a Waganda waliofunga safari kutoka Uganda na usafiri wao wa basi lililoandikwa .Friends’  walimvania dereva huyo na kumnyanyua juu huku wakipeperusha bedera ya nchi yao.

Ifahamike mashindao hayo yalikuwa na vipengere tofauti ambapo kipengere cha kwanza Mganda huyo umeibuka mshindi,badae Mtandao huu utarusha picha za washindi wengine akiwemo mshindi wa Jumla.

Kama kawaida Mtandao huu umekusanya matukio kibao ya chini ya kapeti miongoni mwa matukio hayo ni dereva pekee wakike Mchanga mkazi wa Morogoro kunyakua nafasi ya 8 na kukabidhiwa zawadi.

Matukio mengine ni vituko vya Msanii nchini Mwijangu ambaye naye aikuwa kivutio kwenye mashindano hayo.

Kwa habari zote hizo  nakusihi uendelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

VITUKO VYA MWEZI JANUARI

  Mwezi uliopita tumeshehelekea Siku Kuu mbili X Mas na Mwaka Mpya.   Mwezi huu dume January tunashehelekea kulipa Ada za Shule na kod...