Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, September 3, 2025

KIJIWE NONGWA. UKIONA KAFUTA BANGO UJUMBE UMEFIKA


                 Nesi Tumain Samwel Juma 'Mrs Shekidele'
Bibi Kete akimisha Kete Dustan Shekidele kwenye mja ya Birthday zake
                    Kamisaa Neema Manesa Enzi za Uhai wake










 Hayati Kete Abdallah 103 akizungumza na Mjukuu wake Dustan Shekidee


Na Mpekunyuzi wa Mitandaoni Dunstan Shekidele.

Kama kawaida mtumishi wako, kila wiki naweka Bando linalonitembeza kwenye Mitandao ya Kijamii kukusanya jumbe mbali mbali.

 

Miongoni mwa jumbe hizo ni za Kuelimisha, Kukosoa na Maneno ya hekima yanayotukumbusha kuwa jirani na Mwenyezi Mungu.

 

Mbali na Mungu ambaye kiuhalisia ndio namba moja huku Wazazi kwa maana ya Baba na Mama wakishika nafasi ya pili.

 

Kama hivyo ndivyo tunapaswa kuwaheshimu, kuwatii na kuwatunza wazazi wetu kama jumbe mbali mbali kwenye mabango zinavyotuhasa.

 

Binafsi namuombe mwenyezi Mungu aendelee kunipa roho ya kuwathamini kuwatii, kuwatunza  wazazi wangu waliokuwa hai na  aliotangulia mbele za haki.

 

Kwa wazazi waliotangulia mbele za haki tunapaswa kuwaombea Dua na sala mara kwa mara sambamba na kudhuru kwenye makaburi yao japo mara moja kwa Mwaka.

 

Kwa unyenyekevu Mkuu Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema tunakuomba uwarehemu Marehemu wetu waliotanguia mbele za haki akiwemo  Hayati baba yangu Mzazi Mzee Peter Zakari Shekidele, Mama yangu Mdogo Afande Neema Manase[Pichani mwenye sale za Polisi] Bibi yangu Mzaa Mama Kipenzi Changu My Numbe Number Mshauri wangu Msiri wangu Hayati Bibi Kete Abdallah Batimayo.

 

Bibi yangu huyu Pichani anayenipa Wosia kwa Lugha ya Kisambaa amefariki dunia 2019 akiwa na umri wa miaka 103, wadau wamtandao huu wanakumbuka vizuri kila Mwaka kwenye kumbukizi yake ya kuzaliwa [Happy Birthday] Wajukuu.Vitukuu na Vilembwe vyake zaidi ya 100 tulimfanyia sherehe kambambe nyumbani kwake Gongo la Mboto, Mombasa Mtaa wa Moshi Baa Jijini Dar es salaam.

 

Pia nawambea Marehemu wote  walitanguia mbele za haki tukimumba Mungu awasamehe makosa yao na awaweke  wanapostahiri kwa namna walivyoishi hapa duniani.

 

Kipekee namumbea Mama yangu Mzazi Tumaini Samwel Juma ‘Mrs Shekidele’ ambaye afya yake si nzuri sana akisumbuliwa na Maradhi. Pichani nilimpeleka kwenye Moja Zanahati za Mkoani Morogoro kama anavyoonekana  akipima ugonjwa wa homa ya matumbo’Typhold’

 

Hata hivyo afya yake bado haijatengemaa kwa sasa yuko jijini Dar es salaam akiendelea na Matibabu tunamuomba Mungu amponye Upesi,

 

Tunakuomba haya Mwenyezi Mungu si kwa kukuradhimisha bali kwa upendo na huruma zako tukifuata maandiko yako yanayosema tusikome kukuomba kwenye shida na raha.

 

Ikumbukwe Miaka ya nyuma Mama Tumaini alikuwa  Muuguzi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, kama anavyoonekana pichani akiwa na sale za kazi na kepu kichwani tunashangaa miaka ya sasa manesi hawava hizi kepu. Kwa upande wake haya Neema yeye aikuwa kigogo wa Polisi Kituo Kikuu cha Polisi Morogoro kabla ya kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Kibaha Mkoani Pwani.

Nawakumbuhsa na kuimbusha nafasi yangu tuwadhamini, tuwatunze na tuwatii wazazi wetu, hata kama unacheo,utajiri, Umaarufu vyote hivyo havina dhamani mbele ya wazazi wako waliokuzaa, kukulea na kukusomesha mpaka umefika hapo ulipo, si kwa ujanja wako bali ni Kwa Rehema za mwenyezi Mungu na malezi ya wazazi wako.

 

Tukutane Wiki Ijayo kwa mabango Mengine yenye Jumbe Moto Moto.

No comments:

Post a Comment

VITUKO VYA MWEZI JANUARI

  Mwezi uliopita tumeshehelekea Siku Kuu mbili X Mas na Mwaka Mpya.   Mwezi huu dume January tunashehelekea kulipa Ada za Shule na kod...