Baadhi ya Waandishi wa habari akiwemo Mwandishi wa Mtandao huu mwenye shati la Njano wakifuatilia kwa umakini Mafunzo hayo
Mwenyekiti wa Baraza Profesa Otieno
Afisa wa Baraza Ndahani Msigwa
Msajiri wa Baraza ucy Mziray
Na Dustan Shekidele, Morogoro.
UONGOZI wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala[TAHPC]limebainisha makosa yanayotakiwa kuepukwa na waganga na wakunga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala ili kukwepa adhabu.
Wakionekana hawataki mchezo kwenye ishu hiyo ya kusimamia afya za wananchi, Uongozi mpya wa baraza hilo chini ya Mwenyekiti wake aliyeteuliwa na Mhe Rais Samia Suhuru Hassan[SSH] Profesa Joseph Otieno
Wameamua kutoa Mafunzo ya siku Moja kwa Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro wakiwakumbusha wahusika wote umuhimu wa kuzingatia sheria na miongozo ya Baraza hilo
Sheria hizo zinawagusa moja kwa moja Wanganga,Wakunga Waandishi wa habari, Vyombo vya habari na Mitandao ya Kijamii.
Katika mafunzo hayo yaliofanyika Wiki iliyopita Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine[SUA] Afisa wa Baraza hilo Ndahuni Msigwa alisema Kwamba.
Mganga na Mkunga lazima awe na kituo cha kufanyia shughuri zake. kituo hicho kinaweza kuwa Kilinge.Clinick.Zahanati.Kituo cha Afya au Hospital.
Akifafanua zaidi Msigwa alisema kwenye vituo hivyo wenye kibari cha kulaza wagonjwa ni Kituo cha Afya na Hospital.
“Mfano nyinyi hapa Morogoro Mnakituo cha Afya cha Tiba Asili cha Dr Kisomi ambaye ni bingwa wa kuunga mifupa ya binadamu,kama baraza tunakitambua kituo chake na amekidhi vigezo vya kulaza Wagonjwa.
Kwenye vituo vyote hivyo ni lazima muhusika azingatie usiri na Usitirifu wa Wagonjwa wake,
Azingatie Usafi wake binafsi,Vyombo na Sehemu anayotolea huduma”alisema Afisa huyo wa Baraza na kuongeza kudadavua makatazo hayo.
“Mgonjwa chini ya miaka 18 ahudumiwe mbele ya Mzazi.Ndugu au Mlezi aliyemtu mzima.
Kumpima mgonjwa wa Jinsia tofauti aliyechini ya miaka 18 lazima awepo Mzazi,Ndugu wa Mgonjwa au Msaizidizi wa Jinsia Moja”Alisema Msigwa
MAZUIO MENGINE
Kutoa dawa zilizotengenezwa kutokana na Viungo vya binadamu.
Marufuku kujihusisha na vitendo vya kumdanganya Mteja ili kupata Utajiri.Mali,au kwa kusudio lolote.
Pili Waganga wote hawatakiwi kujihusisha na Vitendo vinavyo chochea lmani za Kishirikina[Uchawi]
Tatu sheria za Baraza zinazuia pia kwa mganga kutoa kauli za Vitisho na Uongo kwa wateja.mfano mganga anamwambia mteja dawahi hii lazima utapona kau hii sio sahihi.
Kwa upande wake Msajiri wa Baraza hilo Lucy Mziray alisema utafiti unaonyesha zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania wanapougua wanaanza kukimbilia Tiba Mbadala na Tiba Asili kabla ya kwenda kwenye matibabu ya kisasa ya hospital
No comments:
Post a Comment