Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, July 9, 2025

MTAAAMU WA AFYA ATAJA KINYWAJI KINACHOZUIA MTU KUZEEKA UPESI.

             Waandishi wa Habari wakifuatilia mafunzo hayo


               Profesa Otieno akionyesha kikombe cha Tangawizi

 

    

     Na Dustan Shekidele Morogoro. MWENYEKITI wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala[TAHPC], Profesa Joseph Otieno amesema kinywaji cha Tangawizi kinazuia mtu kuzeeka haraka.

 

Profesa huyo aliyasema hayo wiki iliyopita  Mara baada ya kufungua  mafunzo ya Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa Waandishi wa habari wa mkoa wa Morogoro.

 

Mafunzo  hayo ya siku moja yaliyoandaliwa na Baraza hilo lililopo chini ya Wizara ya Afya yamefanyika ukumbi wa Engineering uliopo Makao Makuu ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine[SUA].

 

“Kinywaji cha Tangawizi pamoja na Tiba nyingine pia utafiti unaonyesha inasaidi kuzuia mtu kuzeeka upesi, ukitaka usizeeke upesi kila siku kunywa kikombe hichi kimoja cha Tangawizi”aisema na kuongeza.

 

“Toka kipindi kile cha Colona  kila siku lazima nipate kikombe kimoja cha Tangawizi”alisema Profesa huyo ambaye kabla ya kuteuliwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan[SSH] Kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo  alikuwa Daktari Hospital ya Taifa Muhimbili kwa zaidi ya Miaka 6.

 

Mara baada ya kufungua Mkutano huu,muda wa saa 4 asbuhi wanamafunzo hao walikwenda kunywa chai iliyoandaliwa na Baraza hilo, huko kulikuwa na  Supu .Vitafuno mbali mbali.Chai ya Rangi, Kahawa. Maziwa Fresh na Tangawizi.

 

Mwandishi wa habari hizi alikaa  foreni ya Mwisho kwa lengo la [kikachero]kufanya utafiti wa kuchunguza Waandishi wangapi watatumia Tangawizi.

 

Uchunguzi huo umebaini asilimia 90 ya waandishi na wakufunzi wa Baraza hilo wakiongozwa na Profesa Otieno wamekimbili chupa ya Tangawizi wakiyapa kisogo Maziwa Fresh na Kahawa.

 

Katika hatua nyingine Profesa huyo amesema Massage inayofanywa kwenye Masaloon ya Kike na kiume ile pia ni Tiba Mbadala inayoingia Moja kwa Moja kwenye sheria za Baraza hilo.

 

Amesema yeye na Vijana wake wanajipanga kutoa Elimu kwenye masaloon na baada ya kuwaelimisha wahusika sheria inafuata mkondo wake kwa watakaokwenda kinyume na matakwa ya sheria za Baraza.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro Nickson Mkilanya alipopewa nafasi ya Kusema chochote kabla ya Mafunzo hayo kufungwa alisema haya.

 

“Tunaishukuru serikali kupitia Baraza hili kwa kutoa mafunzo kwa Waandishi wa habari wa Mkoa wa Morogoro.

 

Profesa amekiri kwamba kupia kwa maswali mengi yaliyoulizwa na Waandishi kama Baraza umenufaika sana kiasi cha kufikili kufanya mafunzo kama haya mikoa Mingine.

 

Kwa niaba ya waandishi wa habari nasisi pia tumenufaika sana na mafunzo haya hivyo naweza kusema mafunzo haya yamekuwa win win Stretion[Yametunufaisha sote]”amesema Mkilanya na kupokea zawadi ya makofisi mawili matatu kutoka kwa viongozi wa Baraza hilo.

 

No comments:

Post a Comment

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...