Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro Nickson Mkilanya Kushoto akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza hilo Profesa Joseph Otieno.
Wanahabari hao wakiwa wakifuatiia semina hiyo
Na Dustan Shekidele Morogoro.
UONGOZI wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala[TATM] chini ya Mwenyekiti wake Profesa Joseph Otieno wiki iliyopita wametoa semina kwa Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro,wakitolea ufafanuzi wa Mambo mbali mbali ikiwemo ya kisheria na adhabu kwa Vyombo vya habari na waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala wanaokwenda kinyume na sheria za Baraza hilo.
Semina hiyo iliyohudhuriwa pia na Mwandishi wa habari hizi[Pichani mwenye shati la Njano]imefanyika Jumamosi iliyopita Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine[SUA] ukumbi wa Engineering.
Awari mkufunzi wa semina hiyo Martin Magongwa[pichani aiyeketi mbele ya mashine] alitolea Ufafanuzi Maneno ya Tiba Asili na Tiba Mbadala ufafanuzi huo ni kama ifuatavyo.
TIBA ASILI.
Ni jumla ya Maarifa na Utendaji Unaotumika katika Uchunguzi Kinga na Uponyaji wa Matatizo ya Kimwili,Kiakili na Kimahusiano.
Uzowefu huo unaweza kutengeneza uchunguzi unaorithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya Mdomo au Maandishi.
TIBA MBADALA,
Ni jumla ya Maarifa na Utendaji Uliotumika katika Uchunguzi kingaji na Uponyaji wa Matatizo ya Kimwili,Kiakili na Kijamii kwa kutegemea tu Mifumo Mbali mbali iliyoanzishwa na Tiba Mbadala ya Nyanja husika.
Mkufunzi huyo alisema sio sahihi Mganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kuitwa Mganga wa Kienyeji
MUUNDO WA BARAZA HILO.
Mwenyekiti anateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
huku Waziri wa Afya akiteuwa wajumbe 7 ambao ni Waganga 4 wa Tiba Asili,Waganga 2 wa Tiba Mbadala, Mkunga 1 wa Tiba Asili na Mwanasheria 1 kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
MAJUKUMU YA BARAZA
Nikuinda Jamii dhidi ya Matumizi mabaya ya huduma,Waganga wa TATM na Utafiti kwa Mwanadamu.
Kudhibiti Usambazaji wa Habari na Matangazo yote yanayohusiana na TATM.
Kudhibiti na kuweka Viwango inapowezekana kwa huduma na dawa za TATM na huduma Rasirimali Asili na nyingine zenye uwezo wa kuwa dawa.
Alipotakiwa kutoa Takwimu ya adhabu walizota Afisa huyo wa baraza alisema” Wanga 2o waliokiuka sheria za baraza hizo walisimamishwa na 3 walifutiwa Usajiri huku vyombo 3 vya habari vilipigwa faini kwa kukiuksa pia sheria za Baraza hilo.
Amesema uchunguzi wao unanyesha vyombo vya habari vya Mikoa ya Mwanza,Dar es salaamu na Morogoro ndio vinavyoongoza kukiusha sheria za Baraza
Aidha Afisa huyo amesema Simiyu ndio inayoongoza kwa kuwa na Wanga wengi
Kama kawaida Mtandao huu umekusanya habari kibao kwenye semina hiyo ikiwemo bahari ya kinywaji kinachozuia mtu kuzeeka upesi hivyo endele kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment