Madent wa Shule ya Msingi Kaloleleni wakigombea kuvuka kwenye daraja hilo la muda
Muonekana wa sasa baada ya daraja la awari kuondewa
Na Dustan Shekidele.Mogoro
ILI kupata uwanja mpana wa kufanya kasi kwa haraka, wakandarasi wa Kampuni ya COPE iliyopewa jukumu la kujenga daraja kubwa a Relwe Maarufu daraja la Ng’ombe ameamua kuliondoa daraja la zamani na kutengeneza daraja la muda upande wa kulia wa Mto Morogoro.
Ikumbukwe mwezi ulipita daraja hilo lilikatika na kukata mawasiliano ya watumiaji wa daraja hilo wananchi wa kata za Mji Mpya na o Kichangani.
Hali hiyo ilisababisha usumbufu kwa watu mball ikiwemo wanafunzi wa shule za Sekondari na Msingi pamoja na wazee wasiojiweza wanaotunzwa na serikali kwenye kambi ya Funga funga.
Juzi Mtandao huu ulitinga kwenye daraja hilo kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo na kuwahabarisha wananchi hususani wananchi wa kata za Mji Mpya na Kichangani wanautumia daraja hilo ambalo ni kiunganishi muhimu cha kata hizo mbili ambazo ni Maarufu Mkoani Morogoro.
Baada ya kufika Mtaa wa Makaburi ‘A’ kata ya Mji Mpya lilipo daraja hilo Mtandao huu ulishuhudia watu mbali mbali wakiwemo wanafunzi wa shule ya Msingi Kaloleni wakigombea kuvuka kwenye daraja la Muda kama wanavyoonekana pichani.
Wahenga wanasema ‘kujisifu sio dhambi dhambi ni kuziendekeza hizo sifa’.
Mara baada ya daraja hilo kukatika Mtandao ndio ulikuwa wa kwanza kuripotia habari hiyo.sasa hapa siziendekezi hizo sifa ndio maana naendele kuwapa mwendelezo wa ujenzzi wa daraja hilo mara kwa Mara.
Mtandao huu utafanya hivyo mpaka daraja hilo litakapokamiika.
No comments:
Post a Comment