Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, July 2, 2025

BREKING NEWS SIMBA MORO,WASHIRIKI DUA NA SHEREHE ZA YANGA KUTWAA UBINGWA







 

             

         Na Dustan Shekidele, Morogoro.

UKISTAAJABU ya Musa hutoyaona ya Filahuni. Viongozi wa Matawi ya Simba Mkoa wa Morogoro  wamehudhuria Dua iliyokwenda sambamba na sherehe za Yanga kutwaa Vikombe 5 na kumfunga Mtani wao Simba mara 5 mfurulizo.

Shughuri hizo mbili kwa Mpigo zilizohudhuriwa na Shehe Mkuu wa Kata ya Mji Mpya Shehe Kassimu, Diwani wa Kata ya Mji Mpya Mhe Emmy Kiula  na Viongozi Wa Simba zimefanyika jana  ndani ya Tawi kuu a Yanga Mkoa wa Morogoro lililopo Mtaa wa Fumilwa A Kata ya Mji Mpya Mkoani hapa.

Viongozi wa tawi hilo walimtwangia Simu Mmiliki wa Mtandao huu ambaye fasta alitinga kwenye tawi hilo na kushuhudia Shehe kasimu kwa kushirikiana na Mashehe wa Msikingi wa Kingo kwa pamoja wakiongoza dua la kuwarehemu Viongozi na Wafadhiri wa Yanga waliotangulia Mbele za haki.

Viongozi na wafadhiri hao  ni Mzee Karume. Mzee Matunda. Mzee Tabu Mangala na Mzee Madega.

Kwa upande wa wafadhiri ni Abass Gulamari’Mwana wa Pakaya kutoka lfakara Mzee Mengi wa IPP na Manji.

wengine walio rehemiwa kwenye dua hiyo ni wanachama na wapenzi wa yanga waliofariki Dunia.

Baada ya dua  wanayanga na wageni wao Simba walikunya miguu na kupokea sadaka ya chakua cha ‘Mtume’ Wali mweupe na Pilau’ikisindikizwa na kitoweo ‘Nyama’

Viongozi wa Simba walioshuhudiwa na Mtandao huu ndani ya tawi hilo la Yanga ni Mwenyekiti wa Matawi yote ya Simba Mkoa wa Morogoro Mhe Said Mkwinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa C ‘B’  Kata ya Mji Mpya, Waasisi wa timu ya shujaa na tawi la  Shujaa ndugu wa Simba Mzee Mseremu na Mzee Kiwamba pamoja na Mwanachama lia lia wa Simba Mzee Zuberi Mlanzi.

 KIPENGELE CHA PILI CHA SHEREHE,SIMBA WATIMUA MBIO.

Baada ya kutamatika kwa dua na sadaka kiliingia kipengele cha pili cha Wana Yanga kufunga  Muziki Mnene wa Mtaani Maarufu ‘kigodoro’wakifurahia timu yao kumfunga Mtani wao Simba mara 5 sambamba na kunyakua Makombe matano ndani na nje ya Mipaka ya Tanzania.

 

Mtandao huu ulishuhudia Viongozi hao wa Simba wakinyanyuka na kuondoka,kuna hivyo Dj Faraji aliyekuwa kwenye mashine akiwasindikiza na wimbo wa Konde Boy Harmonize wenye maudhui yanayosema

 

‘Waambieni Majirani Yanga Sio Saizi Yao’

 

Mtandao huu ulimfuata Mwenyekiti Mkwinda na kuzungumza naye msikie alichsema” Mpira sio uadui, Mwaliko wa Yanga kwetu walituomba kushiriki kwenye duwa ya kuwarehemu Viongozi wao. Sasa shekidee hapo kuna ubaya?

 

Kweli baada ya dua kutamatika tumeufinya mpunga baada ya kumaliza kula tumeondoka zetu tumewaachia sherehe yao kimsingi hatukuarikwa kwenye sherehe kama mwalikoungesomeka hivyo tusingekuja”alisema Mkwinda

Kwa Upande wake Mwenyeki wa tawi a Yanga Mhe Issa Kitukwa      Maarufu Issa ‘Chabala’ambaye pia ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Fumilwa A alisema

 

“ Tunashukuru shughuri yetu imekwisha salama kipekee niwashukuru Mashehe waliongozwa na shehe wa Kata, nimshukuru Mhe Diwani Mama Kiula ambaye pia ni kiongozi wa tawi hili

 

Niwashukuru watani zetu simba kuitikia mwaliko wetu niwashukuru wanayanga waliojitokeza kwa wingi, mwisho nikushukuru wewe shekidele pia kwa kuitikia Mwalikowetu” alisema mwenyekiti huyo pichani mwenye sahani wa wali.

 

Shughuri hiyo pia imehudhuriwa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Yanga kutoka  tawi hilo Mzee Alon Temu ambaye ni Afisa Utamaduni na Michezo Manispaa ya Morogoro kwa sasa Mzee huyo pichani anayetembelea fimbo amestaafu kazi hiyo ya utumishi serikalini anajukumua moja la kuwaweka Viongozi wakuu wa Yanga madarakani.

 

No comments:

Post a Comment

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...