Soko la zamani
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
HII inaweza kuwa ni kichekesho, wakati wafanyabiasha wa Soko kuu la Morogoro wengi wao wakifanya biashara zinazuhusiana na Kilimo kinacho hitaji mvua nyingi zitakazomweshesha Mkulima huyo kuvuna mazao Mengi na kuyaingiza sokoni.
Wakati huo huo wafanyabiashara hao wa Soko kuu la Morogoro unapofika msimu wa Mvua[Masika] baadhi yao huchukizwa na msimu huo kufuatia mafurika yanayosababishwa na mvua hizo kuvamia kwenye Soko hilo mara nyingi nyakati za usiku wakati wafanyabiashara ha hawapo.
Wanapfika asubuhi wanakutana na mafuriko yariyosomba bidhaa zao huku baadhi yao huku baadhi yao wakiendesha biashara hizo kwa mitaji ya Mikopo.
Hii nilikuwa ni Mwaka 2015 kushuka chini, mafuriko hayo yalizalishwa na mto kikundi uliokatiza katikati ya Mji kando ya Soko hilo ambalo limejengwa Mwaka 1953.
Nakumbuka kufuatia kero ya Mto huo Mbunge mmoja wa Jimbo la Morogoro[tunamuhifadhi jina] kwenye moja ya michango yake bungeni aliiomba serikali kuhamisha mto huo usikatize katikati ya Mji wa Morogoro.
Mwaka 2017 Serikali ililivunja soko hilo nakujenga Soko la Kisasa la Ghorofa kama linavyoonekama pichani,baada ya kukamilika lilipewa jina la Chifu wa Kabila la Waluguru [Soko Kuu la Chifu Kingalu]
Kwa sasa Mtandao huu umeshuhudia mafundi wakiendele na kazi ya kuutanua Mto huo wa Kikundi sambama na kuujenga kwa maweze lengo kuu kuthibiti mafuriko yanayozalishwa na mto huo unaopokeka maji toka juu ya Milima ya Uluguru.
Mtoto wa 2000 unajua kwamba kwenye soko hilo la zamani upande wa Bank ya NMB la kuu la kuingia sokoni hapo lilikuwa likiitwa lako la Jiji?.
lkumbukwe unapoingia kwenye lako hilo kushoto alikuwepo bingwa wa kuchoma Mishikaki aliyefahamika kwa jina la [Jeta Mishikaki]
Huyu jamaa mishikaki yake ilikuwa mitamu sana jioni wahindi na waarabu wakifunga maduka ya mtoko wao ulikuwa kwa Jeta Mishikaki wakifuata mishikaki, Chipsi, Ndizi Choma na chachando tamu tamu.
Kwa sasa mkali wa kuchoma Mishikaki,Chipsi na Ndizi Choma Mkoa wa Morogoro ni Rafiki yangu Mzige Makamba huyu jamaa anapatikana chini ya Mkungu nje ya baa ya Kambarage iliyopo mzunguko wa barabara ya SUA.
Kufuatia utamu wa Mishikaki ya Mzinge Makamba miezi ya hivi karibuni amefungua ofisi nyingine Jijini Dodoma,akitekeleza maombi ya wateja wake wakiwemo waheshimiwa wakiongozwa na Mbunge wa Bumbuli Mhe January Makamba, ambao wengi wao wanapotoka Dodoma kwenda Dar ukatiza kambarage kutafuna mishikaki hiyo.
Akizungumza na Mtandao huu ‘Big Boss’ Nzinge Makamba amesema baada ya kufungua gori Dodoma kwa sasa yuko mbioni kufungua ofisi nyingine Dar es salaam.












