Na Dustan Shekidele,Morogoro.
MTETEZI wawanyonge Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini,Mhe Abdulazizi Mohamed Abood Maarufu [ Azizi Abood] Mara zote ameoneka kuwa jirani na wananchi wa Jimbo lake kwenye shida na raha.
Mhe Abood ambaye anatajwa kuwa tajiri namba moja mkoa wa Morogoro akimiliki Viwanda, Maduka, Vituo vya Mafuta, Vyombo vya habari[Abood Media] Malori na Mabasi yanayofanya safari mikoa mbali mbali ya Tanzania.
Mbali na Utajiri huo lakini linapofika swala la wananchi wa jimbo lake utajiri wake anauweza kando na kujichanganya na wananchi wao, kama wamekaa kwenye vumbi naye anakaa kwenye vumbu kama wanafanya ujasiria mali wa kusokota Chapati naye anasokota chapati kama wanacheza Ngoma naye anasakata Rhumba.
Hivi karibuni katika hatua ya kutekeleza wa Ilani ya chama cha Mapinduzi [CCM] ya uwezeshaji wananchi Kiuchumi 2000-2025.
Kuelekea utekelezaji wa ilani hiyo kiasi cha shilingi Bilion 2,171,359,000,00 zimetolewa kwa vikundi mbali mbali vya Jimbo la Morogoro kama asilimia 10 ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Vikundi vilivyofaidika na pesa hizo ni Vikundi 127 vya wanaume vilivyokopeswa Bilion 1,298,496,000,00.
Vikundi 56 vya Vijana vimekopeswa Milion 723,013,000,00 na Vikundi 19 vya Walemavu nimekopeswa Milion 149.850.000.00.
Kama hiyo haitoshi Mtandao huu ulimnasa Mbunge huyo akizunguka mitaani na miguu akisikiliza changamoto za wananchi wanaofanya shughuri ya kuomba omba mitaani siku za ljumaa na jumapili.
lfahamike hata kabla ya hajawa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Azizi kwa zaidi ya miaka 20 mfurulizo amekuwa akitoa mabasi yake kwenye shughuri za misiba kwa wananchi wa Jimbo la Morogoro huduma hiyo alianza kuitoka Mwaka 2000 mpasa sasa inaendelea.
No comments:
Post a Comment