Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, June 13, 2025

YALIYOJIRI KUMBI ZA STAREHE MWISHONI MWA WEKI MPIGA TARUMBETA SIKINDE AIBUKIA WAUGURU OG












                      Makelele na Mtembezi wakipoliza Tarumbeta


 Na Mlala Nje Dustan Shekidele Morogoro.

MPIGA Trambeti wa Band Kongwe nchini  Mlimani Park Orchestra Maarufu ‘Sikinde Ngoma ya Ukae’ yenye maskani yake Jijini Dar es salam Said Makelele ameibukia band ya ‘Waluguru Original’ ya Mkoani Morogoro

 

Kama kawaida Mlala Nje akiwa kwenye kipengele chake cha kuzunguka kumbi za Starehe kila ‘Week End’kusaka Matukio,ljumaa iliyopita Majira ya saa 6 usiku alitua Ukumbi wa Terminal Msamvu na kumshuhudia Makelele mwenye suti Nyeusi akiwa na band ya Waluguru Og akipuliza Trambeti akishiriki kuimba wimbo  ‘Copy’ wa Jojina.

 

Mara baada ya Makelele kumuona Mlala Nje ana mtwanga Mapicha aliangua kicheko, lfahameke Makelele kabla ya kutimkia Dar  alikuwa Morogoro kikundi cha Matarumbeta cha Mango Garden kinachotoa huduma kwenye sherehe mbali mbali kama vile Harusi na Send Off hivyo Mara kwa Mara Mpiga Picha Maarufu wa Mtandao huu alikutana na Makelele kwenye sherehe hizo.

 

Baada ya  Mwanamuziki huyo kushuka Jukwaani Mlala Nje alizungumza naye.

”Bado niko Sikinde hapa Moro ni nyumbani Shekidele nimekuja kuwasalimia  ndugu zangu week End hii nimeona nije kuwapa campany band yetu Pendwa ya Waluguru Og jumatatu Mungu akipenda naludi Dar”alisema Makelele.

 

Waluguru Og inayomilikiwa na Deograsiasy Makalla Maarufu ‘Killer Boy’inampiga Trambeti mmoja Mohamed Mtembezi[Pichani anayepiga Tarumbeta na Makelele

No comments:

Post a Comment

MTETEZI WAWANYONGE AKALIA VUMBI AKISIKILIZA SHIDA ZA WANANCHI WAKE.

                            Mhe Abood akiketi chini ya vumbi                                 Na Dustan Shekidele,Morogoro. MTETEZI wawan...