Nyomi ya watu iliyofurika jana uwanja wa Saba saba kwa kiingilio cha elfu 2
Beki wa Black baada ya kuiga kichwa mira uliteleza na kutambaa kwenye mkono ndani ya boksi hata hivyo Mwamuzi wa mchezo huo Selemani Kingu gani na msaidizi wake Line One Rajabu Yek yeke hawakuona tukio hilo.
Ama wameona wametafsiri mpira umefuata mkono na kuamua kuimeza firimbi kazi ikaendelea.
Shabiki wa Damu Chafu wakiwa na bango lao lenye jumbe mbali mbliai
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
TIMU ya Damu Chafu yenye maskani yake Pande za Mafisa Kata ya Mwembesongo mkoani hapa, wametinga Fainali ya Michuano ya Ndondo Cup, baada ya kuwadhibu Mahasimu wao wakubwa Black People’Taifa la Watu weusi’ kutoka Jijiga Kaloleni Kata ya Mji Mpya.
Vijana hao wa Damu Chafu wanaopigwa tafu na Mtanzani anayecheza Soka la Kulipwa barani Ulaya Kelvin John’Mbappe’wamefanya hivyo baada ya kuibuka na ushindi wa pelnati 3 dhidi ya 2 za Black People baada ya timu hizo kutoka suluhu -0-0 kwenye mchezo huo uliopigwa jana Uwanja wa Saba saba.
Ifahamike Kelvin John amezaliwa na kukulia eneo hilo la Mafisa ambapo nyumbani kwao ni jirani kabisa na maskani ya Damu Chafu,inayoongozwa na Rais Ayub.
Ikumbukwe Damu chafu ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo ya Planet Ndondo Cup, baada ya kutwaa ubingwa huo mwaka jana wakiwa na beki kisiki wa Simba Abdulrazack Spear Hamza aliyetokea timu ya Super Sport inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Mara baada ya mchezo huo wa fainali kutamatika Hamza alitimkia Dar na kusajiriwa na Simba anayoitumikia mpaka sasa akiwa beki kitegeo.
Kama kawaida Mtandao huu umekusanya matukio kibao kwenye mchezo huo wa jana hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote kuangalia matukio hayo ya ndani na nje ya uwanja ikiwemo tukio la uhodari wa makipa wa timu zote mbili kudaka Pelnati .
No comments:
Post a Comment