Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Kama ilivyoada ya Mtandao huu kufuatilia jambo hatua kwa hatu mpaka hitimisho.
Baada ya jana kuripoti habari ya daraja la watembea kwa miguu la Relwe Maarufu daraja a Ng’ombe kukatika na kusababisha watumiaji wa daraja hilo yakiwemo wakundi ya watu wenye uhitaji maalumu kama vile wanafunzi wa shule za Msingi za Kaloleni, Bungo. Mwere A na B, Mchikichini A na B na Nguzo English Medium.
Nyingine ni Shule za Sekondari za Kingurunyembe. Forest Hill. Morogoro Sekondari na Chuo cha Ufundi Stad ‘VETA’.
Ifahamike licha ya shule kufungwa wanafunzi wa darasa la Nne, La saba. Kidato cha pili na cha Nne wao wanaendeea kwenda shule kufuatia madarasa hayo kukabiiwa na mitihani ya Taifa.
Kundi lingine lenye uhitaji ni Wazee wa wasiojiweza wanaolelewa na Serikali katika kambi ya Funga Funga iliyopo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambayo iko Ng’ambo ya daraja hilo na eneo hilo hakuna mahitaji yoyote ya kijamii kama vile maduka, na masoko, huduma hizo ziko ng’ambo ya pili ya daraja.
Leo Mwandishi wa habari hizi alitinga eneo hilo kwa lengo kufuatilia ‘sako kwa bako’ kama daraja la muda limetengenezwa kama alivyoahidi mmoja wa Makandarasi wanaojenge daraja Jipya.
Mtandao huu umeshuhudia ahadi hiyo ikitekelezwa na Muda huu Mwanahabari huyo anawashuhudia wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wakivuka daraja hilo mmoja akitoka shule ya Msingi na mwingine akielekea shule ya Sekondari ‘Moro Seko’ na usafiri wake wa baiskeri
No comments:
Post a Comment