Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, June 16, 2025

WANAWAKE NA WANAUME WATWANGANA MAKONDE NUSU FAINAL YA NDONDO CUP.


Rais wa timu ya Damu Chafu Ayub mwenye nguo nyeusi kati akiwa na mashabiki wake wakizunguka uwanja was aba saba na kispika chao.

Baade mmoja wa moja wa mashabiki hao mwenye flana ya rangi ya bahari kushoto alizichapa na shabiki mmoja wa Black Peole.

 

        Mashabiki wa kike wakitwangana makonde kavu kavu
                      Mashabiki wa kiume wakitwangana makonde



 


     Na Dustan Shekidele,Morogoro.

YALIYOJIRI Nje ya Uwanja Nusu Fainali ya Michuano ya Planet Ndondo Cup, mashabiki wa kike na kiume wa timu za Black People na Damu  Chafu wametwangana makonde.

Matukio hayo mawili yametokea dakika ya 75 na 80 ya mchezo huo uliozikutanisha timu hizo zinazotoka maeneo jirani, Black People ‘Taifa la Watu Weusi’ Maskani yao ni Kaloleni ‘Jijiga’ Kata ya Mji Mpya huku Damu Chafu wakitokea Mafisa jirani na shule ya Msingi Mafisa Kata ya Mwembesongo.

 Umbari wa meneo hayo ni kama mita 40 sawa na urefu wa viwanja 4 vya mpira hivyo ni majirani wanaofahamiana vizuri.

CHANZO CHA UGOMVI HAKIJAFAHAMIKLA MARA MOJA.

Dakika ya 75 Mwandishi wa habari hizi aliwashuhudia wanawake wawili wakitwangana makonde mmoja akidaiwa shabiki wa Damu Mchafu na Mwingine wa Black People.

 

Mara baada ya mademu hao kuamuliwa na kutulia  chaajabu dakika 5 mbele eneo hilo hilo zikaibuka ngumi nyingine safari hii ni za mashabiki wa kiume wa Black People na Damu Chafu.

 

Chakuchekesha kwenye ugomvi  wa mademu wanaume hao walikuwa mstari wa mbele kuwaamulia baadae wamepishana kiswahiri na kuanza kuchapana makonde.

 

 Vijana wa RPC Alex Mkama waliokuwa Uwanjani hapo wakilinda  Aman na usalama  fasta walifika eneo la tukio na kutuliza ghasia hiyo na mchezo ukaendelea.

Vulugu hizo zilitokea nyuma ya gori la Kaskani mwa Uwanja wa Saba saba ambalo Mwandishi wa habari hizi alikuwa eneo hilo na kamera yake ya kisasa yenye uwezo wa kupiga picha umbali wa mita 300 akikusanya matukio  yote ya ndani nje ya uwanja.   

               


No comments:

Post a Comment

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...