Na Dustan Shekidee Morogoro
HUENDA Ukichezesha Michuano ya Ndondo Cup ni lazima na wewe Refa uwe Mtemi, hii imedhihirika ljumaa iliyopita kwenye Michuano ya Planet Ndondo Cup kati ya Black People’Taifa la Watu Weuzi’ kutoka Kata ya Mji Mpya inayoongozwa na Diwani Mhe, Ummy Kiula na Damu Chafu’ Vijana wa Kelvin John ‘Mbappe’kutoka Kata ya Mwembesongo inayoongozwa na Mhe Ally Kalungwana Maarufu ‘Ally Nyau.’
Katika gemu hiyo ya Nusu fainali ya kwanza ya Michuano ya Ndondo Cup iliyoandaiwa na kituo cha Redio Planet cha Mkoani hapa.imeshuhudiwa Mwamuzi wa mchezo huo Selemani Kinugani akinyoosheana vidole vya shari na baadhi ya mashabiki wa Black People waliongozwa na Rais wa timu hiyo Seif Kijiji mwenye Sing Lend [flana ya ndani] kulia.
Mashabiki hao walilalamikia mchezaji wao kupigwa kiwiko[Kipepsi] na mchezaji wa Damu chafu na Mwamuzi huyo wa zamani wa Ligi kuu kutopuliza firimbi hali iliyowakasirisha Mashabikia hao
Baada ya kuona mchezaji wa anagaragara chini akiuguia maumivu masela hao walivamia uwanja na kumnyooshea vidole refa huku wakimtolea maneno ya Shombo. refa huyo naye hakuwa mnyonge alijibu mapigo yote mawili ya kujibu maneno hayo ya shombo na kuwanyooshea vidole hali hiyo ya kujiamini kwa refa hiyo iliwaogopesha baadhi ya mashabiki hao.
Baada ya kuona hali inazidi kuchafuka Seif Kijiji aliwatuliza Vijana wake akawatoa nje ya Uwanja na baada ya mchezaji wake kutibiwa na kurejea uwanjani gemu hiyo iiyojaza umati mkubwa wawatu iliendelea.
Michuano hiyo mifupi inajumla ya timu 4 pekee zilizoanza hatua ya Nusu fainali timu hizo ni Black People. Damu Chafu. Wakushi kutoka Mtaa wa Manzese Kata ya Mafiga na Chaka Bovu Kutoka Mtaa wa Chuo cha Ujenzi Kata ya Kiwanja Cha Ndege
Nusu fainali ya pili kati ya Wakushi Fc na Chaka Bovu Fc itapigwa mwishoni Mwa wiki hii kwenye uwanja wa CCM Saba saba
HAYA sio yale matwako 4 ya Yanga ya kuelekea Dabi.
Ni shabiki wa timu ya Damu Chafu Fc akiwa mbele ya Kamera za Mtandao huu akionyesha vidole 4 akiashiria timu yake ltaibuka na ushindi wa bao 4-0 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Black People.
Hata hivyo utabili huo haukutimia kwani muda wa dakika 90 timu hizo zilitoka sale o-o na zilipoingia kwenye kipengele cha Mikwaju ya penalty Damu Chafu waliibuka na ushindi wa penati 3-2 na kufanikiwa kutinga Fainali ya michuano hiyo ya Planet Ndondo Cup.
Picha zote na Dustan Shekidele,Morogoro.
No comments:
Post a Comment