.....kbala ya kuvuka kaangalia kulia na kushoto kama kuna gari linakuja
....Baada ya kuona hakuna gari wala boda boda Mbuzi hao wakivuka kwenye Zebra
....Baada ya kufika katikati ya Zebra Bajaj na Boda boda zilisimama kusubiri Mbuzi hao wavuke
Na Dustan Shekidee,Morogoro
UKISTAAJABU ya Mussa huto yaona ya Firahuni.
Msemo huo umetimia juzi baada ya wananchi wa Mtaa wa Manzese Kata ya Misufini Mkoani hapa.kushuhudia Mbuzi wanaojichunga wenye kivuka kwenye kivuko cha watembea kwa miguu Zebra wakitii sharia bila shuruti.
Tukio hilo la kushangaza liloshuhudiwa Live bila chenga na Mwandishi wa habari hizi limetokea Jumanne iliyopita kwenye Zebra hiyo iliyopo barabara ya Kenyata.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo Asha Athumani na Joseph Msimbe walipo hojiwa na Mtandao huu walisema
“ Kila siku tuna washangaa hawa Mbuzi Wanaoishi Manzese jirana na kilabu cha Pombe za kienyeji cha Manzese, wanapotoka Mjini kwenye mihangaiko yao ya kusaka riziki majira ya jioni wanaporejea nyumbani kuna njia nyingi za kufika kwao wanakwepa kugongwa na Magari wanakuja hapa kwenye Zebra kana unavyowaona wanaangalia kulia na kushoto kisha wanavuka kama unavyoshuhudia vyombo vya moto vimesimama kuwapisha wapite”wamesema mashuhuda hao huku wakiangua vicheko
Uongozi wa serikali ya Mkoa wa Morogoro umeamua kuweka zebra eneo hilo kufuatia mzongamano mkubwa wa magari,Bajaji, Boda boda na watu wanaotembea kwa Miguu.
Barabara hiyo inatoka Mnada wa kikundi unapofanyika Mnada mkubwa kila Jumamosi ikielekea Mnada wa Saba saba unaofanyika kila Jumapili.inapofanyikia minada hii njia ya Kikundi na Saba saba inafungwa kupisha minada hiyo inyaonza saa 1 asubuhi mpaka saa 1 jioni
Siku ya Minada hiyo kuna kuwa na msongamano mkubwa wawatu, magari. Bajaj na Boda boda, kufuatia hali hiyo serikali ya Mkoa iliamua kuweka vivuko Zebra kwenye maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment