Na Dustan Shekidele,Morogoro.
JOTO la fainali ya Michuano ya Planet Ndondo Cup linazidi kupanda, baada ya wanafainali timu ya Damu Chafu kunaswa na Mtandao huu wakipiga dua wakimumba Mwenyezi Mungu awajalie kutwaa kombe hilo linalokwenda sambamba na mkwanja kirefu cha pesa.
Mwandisha wa habari hizi akiwa kwenye pilika pilika zake za kusaka habari mitaani jana jioni alikatiza maskani ya timu hiyo Mafisa jirani na geti la kuu la shule ya Msingi Mafisa A na kushuhudia Rais wa timu hiyo mwamba Ayub[kati] mstari wa chini waliochutama akiwaongoza vijana wake kupiga dua la kumuomba Mungu awafanyie wepesi kwenye fainali.
Taarifa zilizopo ambazo hazikuthibitishwa na waandaji wa michuano hiyo zinadai Bigwa atanyakua kombe na pesa taslim Milion 3 huku mshindi wa pili akiondoka na milioni 2.
Leo Ijumaa inapigwa nusu fainali ya pili kati ya Wakushi Fc na Chaka Bovu Fc, kumtafuta mshindi atakayecheza fainali na Damu Chafu June 27 kwenye michuano hiyo iliyoandaliwa na kituo cha Planet Radio.
Ifahamike michuano hiyo inayofanyika kila ijumaa uwanja wa Saba saba Mkoani hapa haina mshindi wa 3, wala wa wane.
No comments:
Post a Comment