Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, June 7, 2025

KWELI DUNIA HAINA HURUMA. MAWENZI MARKET YAISHUHSIA KICHAPO MANGOLO FC AKIOMBOLEZA KIFO CHA MCHEZAJI WAO.





                                          Nasiri Scobba





HII Ndio Ligi ya Mtaani Ndondo Cup, Shabiki anayedhaniwa kuwa wa Mawenzi akivamia uwanja kwa lengo la kutaka kumpigwa Mwamuzi akimlalamika Refa huyo kutopiga Vilimbi baada ya mchezaji wake kukwatuliwa kwenye tukio hili.






Mwamba  akinyumbulika akitaka kufunga bao la kideo la Tick taka,hata hivyo shoti hilo lilipaa juu ya gori.

   Ggemu ya jana utamu ulikluwa eneo la kiungo Zuberi Dabi kushoto no Staa Mwande kushoto ilikuw ani sako kw abako mwanzo mwenga             

Sccoba

                                         Chegela
                                      George Chota
Kipa wa Mawenzi Geofrey Mmassa anayeitumikia Moro Kids inayoshiriki Ligi daraja la pili akipangua kwa ustadi mkubwa shuti lililopiogwa na mshambuliaji wa Mangolo Fc.



Mikwaju ya Pelnati ya mwisho iliyopigwa na Yunis Dadi wa Mawenzi anayeitumikia timu ya Dar City ya Dar es saalamu inayoshiriki Ligi daraja la pili akipongezwa na mashabiki kwa kufunga pelnati hiyo.
Huku Tarick Tarick jezi no 11 akitoka mjonge baada ya kukosa pelnati ya mwisho.
Picha zote na Dustan Shekidele Morogoro









 

Na Dustan Shekidele,Morogoro.
TIMU ya Mawenzi Market inayomilikiwa na Wafanyabiashara wa Soko la Matunda la Mawenzi la Mkoani hapa, Imetinga fainali ya Michuano ya Ndondo Cup baada ya kuiadhibu timu ya Mangolo Fc iliyokuwa ikiomboleza Msiba wa mchezaji wao Juma Chuma Maarufu ‘Maboga’ aliyefariki dunia miezi kadhaa iliyopita. 
 
Mchezo huo uliokuwa mkali kwa muda wote wa dakika 90 kufuatia timu zote mbili kusheheni wachezaji nyota wa Ligi Kuu,Ligi daraja la kwanza na Ligi daraja la Pili umepigwa jana uwanja wa Saba saba.
Licha ya majonzi waliyokuwa nayo huku baadhi ya mashabiki wakizunguka uwanjani na jezi za Maombolezo zilizoandikwa [R.I.P Juma A Chuma ‘Maboga’] Vijana wa Mangolo Fc kutoka Mwembesongo walipambana kwa lengo la kuchukua kombe hilo kumuenzi Mabonga juhuzi hizo zilizaa matunda na kufanikiwa kuwabana Mawenzi na kutoka hao suluhu ya 0-0.
Kilipoingia Kipengele cha kumtafuta mshindi kwa njia ya Mikwaju ya Pelnati Wauza matunda hao waliibuka kidedea kwa Pelnati 5-4 kufuatia Pelnati ya Mwisho ya Mangolo iliyopigwa na Tarick Tarick [Jezi na 11] kugonga Mwamba wa chini na kurejea uwanja.
Baada ya kukosa ushindi Mwandishi wa habari hizi aliwashuhudia baadhi ya wachezaji wa Mangolo wakiangua Vilio.
lkumbukwe Mawenzi Market miaka ya hivi karibuni ilishiriki Ligi daraja la kwanza Tanzania Bara labla ya kusha na baadae wauza matunda huo kuamua kuiza timu hiyo kwa Mwanasiasa Maarufu Mkoa Singida.
Kwa sasa timu hiyo inacheza michuano ya ligi za Mtaani Maarufu Ndondo Cup, mmoja wa viongozi wa Mawezi alipozungumza na Mtandao huu alisema wanajipanga kuirejesha tena timu hiyo kwenye ulimwengu wa soka.
”Shekidele hii ni salamu tu timu hii inamilikiwa na kitengo cha wauza Kuku pale sokoni tunajiandaa kuisajiri tena kucheza ligi daraja la Nne tunakuja kivingine mpaka Ligi Kuu” alisema kiongozi huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Babuu.
Wakati ikishiri Ligi daraja la Kwanza Mawenzi ilifanikiwa kuzalisha baadhi ya wachezaji nyota kama vile Selemani Mwalimu anayekipiga Wydad ya Morocco. Kipa namba Moja ya Pamba ya Mwanza Yona Amos Omar Baruku’Macello’ Coastal Union ya Tanga.
Baadhi ya wachezaji wa Ligi kuu walioitumikia Mawenzi ni Yona Chegela[Tanzani Prinsons] Omari Manga, George Chota na Chachalo [Mtibwa Sugar]
Kwa upande wa Mangolo ni Richa Mwamba [Mtibwa]Nassiri Kombo’Scoba’ [Tabora United].na Zubery Dabi Mashujaa ya Kigoma.
Zubery mkazi wa Kichangani Mkoani Morogoro anatoka familia ya Mpira, Kaka yake Nassoro Dabi alikiwasha timu ya Polisi Morogoro akafanikiwa kwenda Depo kwa sasa ni Askari Polisi kwenye moja ya Vituo vya Polisi Mkoa wa Morogoro.
Mdogo wake Zubery naye kakiwasha vilivyo Ruvu Shooting ya Pwani akaenda Depo kwa sasa ni Mwanajeshi, Ruvu iliposhuka daraja Zubery katimkia Mashujaa inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania’JWTZ’

No comments:

Post a Comment

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...