Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, June 9, 2025

A-Z DARAJA LA MJI MPYA KUKATIKA.






Mzee  Juma Ulanga akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu jana

 


       Na Dustan Shekidele,Morogoro.

KUFUATIA  kukatika ghafla kwa daraja la watembea kwa miguu la Relwe Maarufu Daraja a Ng’ombe na kukata mawasiliano yaliyoadhiri makundi mengi yenye uhitaji Maalumu.

 

Baadhi ya makundi hayo ni Wazee wasiojiweza wanaolelewa na Serikali kwenye kambi ya Wazee ya ‘Funga Funga’ iliyopo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

 

Kundi la Pili ni la Wanafunzi  hasa wa  darasa la Kwanza.la Pili na la Tatu wa shule za Msingi za Kaloleni. Bungo. Mwere A na B. Mchikichini A na B.

 

 Shule hizo na Kambi hiyo  zote ziko Ng’ambo ya daraja hilo la Ng’ombe. kwa nini linaitwa daraja la Ng’ombe?

 

Mwandishi wa Mtandao huu ambaye alisoma shule ya Msingi Kaloleni miaka hilo akiwa shule  alishuhudia Makundi ya Ng’ombe yakivushwa kwenye daraja hilo kuelekea Stesheni ya Treni iliyopo jirani na daraja hilo.

 

Makundi hayo ya Ng’ombe yalikuwa yakisafirishwa  kuelekea Machinjioni Pugu jijini Dar es salaam.

 

Shule nyingine zilizo Ng’ambo ya daraja hilo ni Shule za Sekondari za  Kigurunyembe, Forest Hill. Morogoro Sekondari, Chuo cha Ufundi Stad ‘VETA’ na hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

 

Licha ya kukatika kwa daraja hilo ifahamike pia kuna njia mbadara ya kufika upande huo wa pili ingawa ni kwa kuzunguka umbari mrefu wa kupita njia ya Nunge.

 

Njia hio sio rafiki sana kwa wanafunzi wa Shule ya Kaloleni na kambi ya Wazee kwa sababu ili kufika maeneo hayo mawili kwa urahisi ni lazima upite juu ya Reli ya Kati inayoelekea Mikoa ya Dodoma, Shinyanga, Tabora Mwanza na Kigoma hivyo kwa mtoto wa la kwanza na mzee wa Miaka 80 kutembe juu ya Reli ni hatari.

 

Mara baada ya daraja hilo kukatika Jana Alfajiri Mkazi wa eneo hilo  Baraka Selaman anayefanya shughuri za kukodisha baiskeri jirani na daraja hilo alimpigia simu Mwandishi wa habari hizi ambaye ndani ya dakika 0 alifika eneo hilo.

 

Kwa vile ilikuwa asubuhi sana hakumkuta kiongozi yoyote eneo hilo hivyo Mwandishi wa habari hizi alipiga picha daraja hilo alipiga Picha na kurusha kwenye Mtandao huu huku akiwasubiri kupambazuke azungumze na watu mbali mbali akiwemo lnjinia wa daraja jipya linalojengwa eneo hilo.

 

Majira ya saa 3 asubuhi Mtandao huu ulifanikiwa kuzungumza na Mzee Maarufu wa eneo hilo  Juma Ulanga.

 

“ Kiukweli daraja hili  linastahiri kukatika lina muda mrefu sana unaona huu umri wangu nimezaliwa nimelikuta, binafsi tunaishukuru serikali kwa kuanza ujezi wa baraja kubwa la kisasa.

 

Lakini licha ya Uzee wa daraja hili tukili ujenzi wa daraja jipya umechangia kukatika kwa hili la zamani kwa sababu wamechimba sana eneo hili la daraja la zamani, ombi letu kwa huyu mkandarasi afungua njia kwa kujenga daraja la Muda ili wanafunzi wa darasa la 4 na 7 ambao hawajafunga shule kesho jumatatu wavuke waende shule.

Pia kuna wale wazee wa Funga funga wamepigwa pini mahitaji yao muhimu yako Ng’ambo hii mfano Soko, na maduka makubwa yako huku”alisema Mzee Ulanga ambaye ana miliki nyumba mbili zilizopo jirani kabisa na daraja hilo lililopo Mtaa wa Makaburi A kata ya Mji Mpya.

 

Baada ya Muda alifika mmoja wa wakandarasi wa kampuni ya COPE wanaojenga daraja hilo jipya ambapo alipohojiwa alikubari kuzungumza kwa sharti la kutotaja jina lake kwa sababu  si msemaji wa kampuni hiyo.

“ Daraja hili tunalojenga ni kwa mahitaji ya wananchi na hili lililokatika pia lilikuwa na mahitaji ya wananchi kuhusu hoja ya kuchimba ni lazima tufanye hivyo kwa sabu tunakwenda na vipimo.

 

Tutakachofanya tutajenga daraja la Muda wananchi waendelee kupita wakati tukiendelea na ujenzi wa daraja hili kubwa la kudumu”aisema Mkandarasi huyo.

No comments:

Post a Comment

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...