Mwandishi wa Mtandao huu akiwa katikati ya Mji wa Morogoro na Chombo yake ya Mwendo Kasi
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
YALIYOJIRI Mitaani Wakala wa Bank na Mitandao ya Simu amenusurika kuporwa mamilioni ya pesa na Vibaka wanaotumia Usafiri wa Pikipiki Maarufu ‘Vishandu.’
Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 1 usiku katika ya Mji wa Morogoro Mtaa wa Uhuru Kata ya Mji Mkuu.
Mara baada ya kutokea kwa tuki hilo baadhi ya mashuhuda walimpigia simu Mwandishi wa habari hizi ambaye fasta alipiga gia Pikipiki yake ya Mwendo Kasi. ndani ya dakika moja alifika eneo la tukio na kukuta Vibaka na wakala huyo wametoweka eneo hilo huku vikundi vya watu vikijadii tukio hilo wengi wao wakimbebesha zigo la uzembe Wakala huyo wa kike.
Paparazi wa habari hizi alivamia kikundi kimoja na kumnyofoa Zumbe Cool ambaye ni bigwa wa zamani wa kusakata Disko Mkoa wa Morogoro. alipotakiwa kuelezea tukio hilo alisema.
”Huyu Wakala licha ya uzembe wake lakini ana bahati, kila siku majira ya saa 1 usiku akifunga ofisi yake anakusanya mapesa anaweka kwenye mfuko wa Magufuli anaondoka na miguu kwenda kupanda daladala stend.
Leo hawa Vibaka wame mtime tunahisi walikuwa 3 mmoja alikuwa pale kwenye kibanda cha uwakala na wawili walikuwa wamebana sehemu na pikipiki wakipokea maelekezo kutoka kwa mwenzao.
Sasa huyu dada alipofunga ofisi kama kawaida yake kaanza kuondoka na miguu huku akiwa na fuko hilo la pesa”alisema shuhuda huyo na kuendelea.
“ Alipofika jirani na hii baa ya Magesho ilikuja pikipiki aina ya TVS Yule aliyepakizwa nyuma alimpora mfuko kama unavyo jua ile Mifuko ya Magufuli ni raini wakati waugombea ulichanika na burugutu la pesa likaanguka chini vibaka wamekimbia na mfuko tupu.
Wakala kaokota mabunda yake ya mapesa aliyoyafunga na rababendi haraka kukodi bajaj kaondoka zake kama unavyoshuhudia vikundi hivi vya watu wanamlaumu huyo Wakala kwa uzembe”alisema Zumbe Cool ambaye ni fundi baiskeli kwenye mtaa huo wa Uhuru.
No comments:
Post a Comment