Twaha Kiduku[Mwenye Flana ya Kijana akichapa kweli kweli na mchezaji mwenzie wa Club ya Moro Boxing
Kocha Pawa lranda [kulia akisimamia mazoezi hayo Picha zote na Dustan Shekidele,Morogoro.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
WADAU wengi wa Ngumi Tanzania kwa sasa wameingia kwenye dibwi kubwa la si mtofahamu baada ya Luninga Maarufu Afrika Azam Tv kusitinga kuonyesha mchezo huo pendwa.
Kundi kubwa la mashabiki wa ngumi hawajua sababu za Azam Tv ‘Wazee wa Burudani kwa wote’kutoonyesha mchezo huo hali iliyopelekea kila mmoja kusema lake.
Taarifa zilizopo zinadai Azam Tv ambao kwa asilimia 90 ndio walioinua mchezo huo wamesitisha kuonyesha masumbwi baada ya bondia mmoja kuishitaki Mahakama.
Kufuatia hali hiyo Mwandishi wa habari hizi amemtafuta bondia maarufu nchini Mwana Morogoro Twaha Kassimu Maarufu Twaha Kiduku ambaye pia ni balozi wa Azam Media kwa lengo la kusikia kauli yake baada ya mabosi wake kusitisa kuonyesha ngumi.
Akizungumza jana jioni mara baada ya kumaliza mazoezi na Klabu yake ya Moro Boxing ndani ya Ukumbi wa Urafiki uliopo Saba saba Mkoani hapa Kiduku ‘Morogoro Finest’ alisema.
”Ni kweli mimi ni balozi wa Azam Media ninamkataba wa miaka 3, kiukweli kitendo cha Azam kutoonyesha mapambano yetu kimetuumiza mabondia wengi hasa mimi balozi.
Hii ni baada ya bondia mwenzetu [anamtaja lina]kuishitaki Azam Media, hali iliyopelekea mabosi wangu wao kusitisha kuonyesha ngumi ”alisema Kiduku
Alipoulizwa kama hivi karibuni ana pambano lolote?, alijibu” Ndio tarehe 24 mwezi huu na cheza na bondia kutoka Malawi jijini Dar es salaam’ Shekidele karibu sana kwenye pambano hilo”alisema Mjuu huyo wa Mamaa wa Misuli Mc Rukia Ndege.
Kwa upande wake Chanzi Mbwana Maarufu ‘Pawa lranda’ambaye ni kocha mkuu wa Bondia Kiduku alisema.
“Azam tv kutoonyesha ngumi kumeathiri wengi wakiwemo Mapromota, mabondia na sisi makocha, bondia anapocheza mechi nyingi mbali na kocha kupata kipato, bado kuna faida ya bondia kupata umaarufu baada ya kuonekana kwenye Tv,
Mfano hapa kwenye klabu yetu ya Moro Boxing tuna vijana wengi wanachipukia wanahitaji sapoti kubwa ya Azam Tv”alisema kocha huyo.
No comments:
Post a Comment