AJALI.
Gari ndogo aina ya Kilikuu limeharibika vibaya eneo la mbele baada ya kudaiwa kuligonga kwa nyuma Lori kubwa ‘Semi’.
Tukio hilo lililoshuhudiwa ‘Live’ na Mpiga picha wa Mtandao huu limetokea jana mchana barabara kuu ya Morogoro- Dar es salaam, jirani na stend ya mabasi ya Msamvu pale pale ulipotokea Mlipuko la Lori la Mfuta Agost 10 -2019 na kua watu zaidi ya 90 wangi wao walikuwa wakigema mafuta kwenye Lori hilo.
Akihojiwa na Mtandao huu dereva wa Lori hilo aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa sababu si msemaji wa kampuni yake alisema.
“ Nasafirisha mabonda haya kutoka Dar kuelekea Dodoma, nilipofika hapa kwenye Zebra’Kivuko cha watembea kwa Miguu nimesimama kupisha wanafunzi wavuke, ghafla nikasikia gari langu kugongwa kwa nyuma” alisema dereva huyo.
Alipoulizwa kinachoendelea kwa sasa ni kipi baada ya kutokea kwa ajali hiyo alijibu.
”Baada ya kukosekana askari eneo hili huyu dereva wa Kili kuu ambaye ndiye Mwenyeji hapa Morogoro nimemuambia aende kituo cha Polisi kuita askari ndio na msubiri aje na polisi wapime anilipe pesa ya kunyoosha gari langu niendelee na safari nikatengeneze gari huko huko mbele kwa sababu mzigo huu unatakiwa kufika leo” alimalizia kusema Dereva huyo.
Kweli changamoto za barabarani ni mwiba mkali, Jama mwenye Kili kuu kwenye ajali hiyo gari lake ndio limeumia sana baada ya kioo cha mbele kuvunjika na bondi na lnjini kuimia, bado dereva huyo wa Kili Kuu anatakiwa kumlipa dereva huyo wa Lori ambaye sehemu ndogo ya nyuma imebonyea.
[Picha na Dustan Shekidele Morogoro].
No comments:
Post a Comment