1. USIJIHUSISHE NA HUSIANO MENGINE KWA LENGO LA KUEPUSHA MIGOGO ISIYO YA LAZIMA ILI KUENDELEA KULINDA MAHUSIANO YAKO NA MWENZI WAKO: Pasitokee MTU mwingine (wa jinsia yeyote) ambaye atakuwa na umuhimu wa juu zaidi kuliko mwenzi wako.
2. USIMLINGANISHE AU KUMSHINDANISHA MWENZI WAKO NA MTU MWINGINE: Kumbuka kila mtu yupo tofauti. Tumia hekima kumfanya mwenzi wako awe bora zaidi pasipo kumfanya ajisikie hafai au hana viwango unavyotaka wewe.Kuwa mbunifu kila siku kwenye mahusiano yako ili yawe mapya siku zote.
3. USITUMIE “TENDO LA NDOA” KAMA FIMBO YA KUMWADHIBU MWENZI WAKO. Hata kama mmepishana misimamo, kumbuka “Tendo la Ndoa” ni haki ya msingi ya kila mwanandoa. Ndio kiini cha nyinyi kuunganishwa kuwa mwili mmoja,kama mmekuwa mwili mmoja hakuna binadamu yoyote anaye chukia sehemu ya kiungo chake mwilini.
4. USIISHI MAISHA YA SIRI KWA MWENZI WAKO. Fanya jitihada za makusudi kuvunja kila tabia ya usiri ambayo itasababisha kila mmoja aishi maisha yake binafsi.kuwa muwazi kwa kila kitu hata ikitokea mwezi wako hayupo uwe na uwezi wa kufungua pini [Namba za Siri] kama vile Bank na kwenye mitandao ya simu.
5. USIJILAUMU KUINGIA KWENYE NDOA AU KUMWONYESHA MWENZI WAKO KWAMBA UNAWEZA PATA MBADALA WAKE WAKATI WOWOTE. Hata kama unahisi “ulikosea kumpata” hayari huo ni msalaba wako ubebe huku ukifanya wajibu wa kuiboresha hiyo ndoa hakuna kinachoshindikana hapa chini ya Juwa. Kumbuka UPENDO una nguvu kuliko MAUTI.
6. USIRUHUSU KAZI AU MAJUKUMU YAKO YAIDHOOFISHE NDOA YAKO: Pamoja na majukumu mengi uliyonayo, hakikisha umuhimu wa ndoa yako unabaki palepale.usiwe bize na majukumu kiasi cha kuisahau familia.
7. USIWE MBINAFSI.Usipendelee mambo yako tu au ndugu zako tu; bali kumbuka pia mwenzi wako naye ana ndugu zake na anamambo yake.hivyo kila jambo unalofanya liwe la uwasa.
8. USIWE MWEPESI KUSAMBAZA MAMBO YENU YA NDANI KWA KILA MTU: Ndoa ni taasisi yenye kanuni na taratibu zake; mojawapo ya kanuni hizo ni “utunzaji wa mambo nyeti” (Confidentiality). Uwe makini unamwambia nani kitu gani. Natambua kwenye ndoa sio pemboni kwamba kila siku utakuw ana furaha na amani ya Moyo, hapa haiku hivyo kuna siku mtakwazana mtachukizani. Ikitokea hali hiyo ukukwaluzana pakubwa kiasi cha kutishia uhai wa ndoa yenu, hivyo kuhitaji usaidizi wa watu wengine.
Kuna watu sahihi wa kuwashirikisha ambao ni wazazi, Wasimamizi wenu wa ndoa{Mashahidi wa ndoa yenu] huko kote ikishindanani basi fikeni kwa viongozi wa dini waliofungisha ndao yenu ambao wana kanuni za mafundisho ya ndoa.
8. USIJIDANGANYE KWAMBA KUNA MTU MWINGINE ANAKUPENDA NA KUKUJALI ZAIDI YA MUME/MKE WAKO: Kumbuka kuna watu wataonyesha wanakujali sana kwa sababu sasa upo kwenye ndoa; siku ukitoka hutaamini kama ndio wale!! watakupita kwa kasi ya ‘SGR’ huku wakikufungia vioo usiwaone.
10. USISAHAU KIAPO CHA NDOA NI KIAPO CHA DAMU… NI KIAPO CHA MAISHA: Usiruhusu mawazo ya kutengana au kuachana yawe RAHISI na MEPESI sana ndani ya kichwa na moyo wako. Mara zote katika changamoto jikumbushe KIAPO CHA NDOA… “Nitakuwa nawe katika hali zote…!!” kubwa zaidi ni kusameahana pale mnapokoseana na kuoweka visasi vya kijinga moyoni ukiamua kusamehe same kweli usihifadhi visasi moyoni.
NYONGEZA.
OMBEA ondea ndoa yako kila mara na ikitoea mtikisiko basi Paleka shida zako kwa MUNGU kabla hujazipeleka kwa Mashoga zako au Marafiki zako hao hawata kusaidia chochote zaidi ya kukutangaza.
No comments:
Post a Comment