Na Dustan Shekidele,Morogoro.
UKISTAAJABU ya Mussa hutoyaona ya firahuni,
Wakati Shule ya Msingi Kaloleni ikijinadi hadharani kusimamia kwa vitendo‘Usafi, Nidhamu na utunzaji Mazingira, hali imekuwa tofauti mazingira ya shule hiyo ni machafu kufuatia kuvamiwa na msitu mkubwa uliozalishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Kufuati hali hiyo Mtandao huu alimtafuta Mwalimu mkuu wa shule hiyo Mikidadi Bakari alipulizwa alisema.
“Ni kweli kauli mbiu yetu ni hiyo angalia tumetunza mazingira kwa kupata miti eneo la shule, kweli kwa sasa kuna hivi vichaka mara nyingi huwa tunawaomba wafungwa wanakuja kutusaidia kufyeka, mvua vinakaribia kwisha nitaenda kuomba wafungwa waje kutufyekea” alisema Mwalimu huyo.
Alipoulizwa kwa nini wanafunzi hawafyeki ili hali huwa mnawaagiza wazazi kununua mafagio na makwanja ya usafi?.
Mwalimu huyo alijibu. Kwetu sisi wanafunzi wako bize na masoma kwa sababu mwisho wa siku watapimwa kwa Taalumu na sio kwa kufyeka
Mwandishi. Nakumbuka wakati nasoma kulikuwa na vipindi vya Masomo.Michezo na Utunzaji mazingira kwa maana ya kufagia na kufyeka, tukipangiwa zamu chini ya usimamizi wa Mwalimu wa zamu.na Mwalimu Mkuu Mama Chausi.
Nakumbuka wakati nasoma hii miti ulikuwepo kama mmepanda mingine basi imefichwa na huu msitu pia nakumbuka kulikuwa na bustani ‘Garden nzuri’ kwa sasa sioni nauona huu msitu mkubwa ambao ni hatari kwa wanafunzi kwanza unaweza kutunza vitu hatarishi kama vile nyoka na Vibaka.
Mwalimu. Kweli unzi wenu na zetu ni tofauti na sasa mambo mengi yamebadilika yako kasi sana tunakimbizana na kasi hiyo hatuna muda wa kupoteza kimasoma.
Ifahamike Mwandishi wa habari hizi alisoma katika shule hiyo la kwanza mpaka la Saba na kwamba miaka ya hivi karibu Mwandishi wa habari hizi alikatiza kwenye shule hiyo na kushuhudia kibao cha shule hiyo kikiporomoka chini.
Kufuatia hali hiyo Mwanahabari huyo alijaribu kuzungumza na baadhi ya wanafunzi wenzie aliomaliza nao la saba akiwemo Galula Jangalu ambaye kaka yake ni Kocha wa zamani wa timu ya Kagera Sugar Ally Jangalu.
Said Mtagwa ambaye naye kaka yake ni mchezaji nyota wa zamani hayati Jella Mtagwa.
Msafiri Salehe Mdule ‘ambaye kwa sasa ni Kigogo wa Ardh Morogoro.
Wengine ni Adam Urasa Mfanyabiashara Maarufu Morogoro akimiliki nyumba za wageni Gest za Mangesho.
Chiku Mwarami. Doto na kulwa Sonny. Mawazo Adamu ambaye kwa sasa ni Mwalimu shule ya Msingi Kinole.
Maneno Mtakahela Fundi Baskeli maeneo ya Mwembesongo. Subira Mkanile na Sawita, Kwa pamoja tulikubalia kufanya kitu kwenye shule kwa lengo la kurejesha fadhira ikiwemo kujenga kibao hicho cha shule.
Neno la kufurahisha jana nilipofika nimeshuhudia kibao kipya kimejengwa kikiwa na kauli mbio hiyo ya ‘Usafi. Nidhamu na Utunzaji Mazingira’ ingawa nacho nilizingira na msitu.
Baada ya mahojiano na Mwalimu huyo nilijivua Uandishi wa habari nikaingia kwenye kipengele kilichonipeleka,nilimuahidi ‘Ticha’ huyo kwamba juhuzi za kuwaunganisha madent wenzangu hao zinaendelea hivyo mchakato utakapokamilika tutafika shuleni hapo na kufanya jambo kwa maslahi mapana ya shule yetu.
No comments:
Post a Comment