Shehe Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Sheikh Jafar Thinei[kushoto anayesoma karatasi]
Mkuu wa wachungaji wa Kanisa a Anglikana Dayosisi ya Morogoro Mchungaji Wilson Mfumbi
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Siku mbili mfurulizo Mtandao Pendwa wa Shekidele umeripoti habari ya kuwasemea walemavu wenye changamoto ya kuongea na kusikia ‘Viziwi’wanakumbana na changamoto kwenye lbada kufuatia nyumba nyingi za ibada kukosa wakalimani wa Lugha za alama.
Hii ni baada ya hivi karibuni Mwandishi wa habari hizi kupokea Manung’uniko kutoka kwa baadhi ya Viziwi wakilalamika kutengwa baada ya nyumba nyingi za lbada kutoweka watu wa kuwasiliana nao.
Baada ya Kupokea Malalamiko hayo mtetezi wawanyonge aliwatafuta Viongozi wa dini zote mbili kwa lengo la kupata majawabu ya Malala miko ya ndugu zetu hao.Wa kwanza kupatikana ni Mkuu Wawachungaji wote wa kanisa la Anglikani Dayosisi ya Morogoro,Mchungaji Wilson Mafumbi ambaye pia ni Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi hiyo.
Mwandishi- Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu
Mchungaji- Amen karibu sana ofisini Mwanahabari wetu.
Mwandishi- Asante, bila kupoteza muda nieleze kiicho nileta wewe kama Mkuu wa wachungaji wa makanisa yote ya Anglikana Dayosisi ya Morogoro kwenye Dayosisi yako Mnawalemavu wangambi wenye changamto za kusikia na kuongea’Viziwi’?
Mchungaji- Wapo wengi ila kujua idadi yao kwa haraka haraka hivi itakuwa ngumu ila ukija siku nyingine naweza kukupa idadi yao.
Mwandishi- Kama umekili wapo tena kwa wingi Je kwenye lbada zenu mnawasiliana nao vipi kwenye Matangazo na mahubiri?
Mchungaji- Nikili kwenye makanisa yetu mengi hakuna wataalamu wa Lugha za alama ambao kimsingi ndio wanaoweza kuwasiliana na waumini wetu hao.
Mwandishi- Nimeradhimika kuja kwako kwa sababu kuna muumini mmoja wa kanisa hili, Kiziwi kwa kukosa mtaaamu wa Lugha za alama alipata shida kubwa kumbatiza Mwanae nyinyi kama wachungaji mliopewa jukumu la kuchunga kwa usawa Kondoo wote wa Mungu kwa nini kwenye uchungaji wetu baadhi yenu kwa kujua ama kwa kuto jua mnawatenga kondoo wenu wenye ulemavu wa kusikia.
Mchungaji- Kwanza nikushukuru sana kwa kutukumbusha hilo kama mkuu wa wachungaji nakili mapungufu hayo
Tukimaiza mahjiano haya nitawasiliana na wachungaji wote tuweke wataalamu wa Lugha za alama kwenye lbada zetu
Hakika kwa hili ulilofanya la kuwasemea Viziwi hata usipopewa Tuzo Duniani naamini kesho kwa Mungu utapata Tuzo tena kubwa, naomba nipe majina ya huyo Kiziwi aliyepata changamoto ya Ubatizo.
Mwandishi- majina haya hapa na wewe naomba nikupige picha hapa ofisini nitumie kwenye stori hii.
Mchungaji. Hapa sijavaa kola ya Uchungaji namba yako ya Whatsapp ninayo nitakutumia picha nyingi nikiwa na kola.
Mwandishi- Asante.
Baada ya kutoka kanisani hapo Mwandishi wa habari hizi alimtwangia simu Shehe Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Shehe Jafar Thinei.
Mwandishi- Asalaam Alaikum Shehe Mkuu wa Wilaya.
Shehe- Aleikum Mwislam, nambiye Shekidele Mwandishi Nguli Morogoro.
Mwandishi- Nipo Shehe wangu swali langu kwako kwenye Wilaya yako unawaumini wangapi wenye ulemavu wa kusikia ‘Viziwi’ na kama wapo wanayapokeaje matangazo na Mawaidha Msikitini?
Shehe- Kwenye Wilaya yangu waumini hao wapo wengi kuhusu kupokea Matangazo na Mawaidha ofisi ya Shehe Mkuu wa Mkoa kuna Mtaalamu mmoja wa Lugha za alama ambaye ofisi ya Shehe wa Mkoa ndio inayompangia kuhudhuria Msikiti wenye waumini wengi Viziwi kwenye Mkoa wa Morogoro.
Binafsi napambana na mimi nipata Mtalamu japo mmoja kwenye Wilaya yangu nashukuru sana umenikumbusha niongeze kasi ya kumtafuta mtaaamu huyo barikiwa sana Shekidele.
Mwandishi. Amina Shehe ijumaa Karim
Shehe Ok ninavyokujua umeshanirekodi tayari
Mwandishi- Mapema sana si umeingia kwenye Mfumo
Shehe- Kicheko kisha amekata simu.
No comments:
Post a Comment