Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, May 10, 2025

SEHEMU YA PILI STORI YA KITAA. ASKOFU ASIGITISHWA MLEMAVU ‘KIZIWI’KUTOJULISHWA TANGAZO LA UBATIZO.

Baraka na familiya yake wakizungumza na Mwandishi wa habari hizi nje ya nyumba hiyo muda mfupi kabla ya  kuelekea kanisani.

 


 

        Na Dustan Shekidele,Morogoro.

 

MPENDWA Msomaji leo tunaingia sehemu ya pili  ya stori kali ya kitaa iliyoanza kuruka hewani juzi.

 

Kwenye stori hiyo tuliishia  kipengele cha kuwaomba Viongozi wa dini Mikoa yote Tanzania  kuweka  wataalamu wa Lugha za alama kwenye lbada zao ili kuwapa haki  ya msingi walemavu ’Viziwi’  kusikia Mahuribi, Mawaidha na Matangazo muhimu yanayotolewa kwenye lbada.

 

   MANUNG’UNIKO YA BAADHI YA VIZIWI.

 

Mwandishi wa habari hizi amejaliwa na  Mungu kupata kibanda cha kuishi ambapo kwenye kibanda hicho pia amejaliwa kupata Mpangaji  Baraka Simon na mkewe Blenda Martin wote ni ’Viziwi’ hawasikii wala kuongea

 

Mwanaume ni mfanyakazi wa SUMA JKT kItengo cha Ujenzi na mkewe ni Mama wa nyumbani, wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kike waliyembatiza kwa jina la Glory ambaye kwa ukuu wa  Mungu sio ‘kiziwi’ anaongea na kusikia.

 

Wanandoa hao waliofunga ndoa kwao Dodoma takribani miaka 7 iliyopita ni waumini wa kanisa kuu la Anglikana lililopo ’Round-About’Mzunguko  wa barabara za SUA.Kenyata. Madaraka na Kingo katikati ya Mji wa Morogoro kila Jumapili hungana na waumini wenzano kumuabudu  Mungu kwenye kanisa hilo.

 

Mara baada ya mtoto huyo kubatizwa baadae Devary Martin ambaye ni shemeji wa Baraka alitoka Dodoma kuja Morogoro kumsalimia dada yake hivyo, Mwandishi wa habari hizi alimtumia kama mkalimani kwenye mahojiano na Baraka.

 

Akisimulia ugumu walioupata kwenye mchakato wa kumbatiza Mwanae  Baraka alisema.

 

“Mimi na mkewe wangu kama unavyotushudia kila jumapili tuna kwenda kanisani, bahati mbaya sana kwenye kanisa letu hakuna mtu tunayewasiliana naye kwa alama za Vidole lakini hilo halituzuii kwenda kumuabudu Mungu wetu ambaye huwa tunawasiliana naye kmya kimya.

 

Kwa kutokuwepo mtaamu wa Lugha za alama  hakuna tunachosikia kwenye lbada  huwa tunafuata mkumbo tu watu wakisimama na sisi tunasimama wakiinuka kutoa sadaka na sisi tunainuka.

 

Changamoto kubwa ni kwenye matangazo  mara nyingi huwa tunapitwa na vitu vingi kanisa mfano linaweza kutoka tangazo la mabadiliko ya saa ya ibada jumapili ijayo sisi hatujui tunakuja muda ule ule wa kawaida hatukuti mtu  basi tunaludi nyumbani”alisema Baraka na kuongeza

 

Kubwa zaidi tumejaliwa kupata huyu mtoto tangazo la ubatizo limetoka siku za nyuma licha ya sisi kuweo kanisa hatukusikia kwa sababu hakuna wa kutuambia jumapili iliyofuata tumeshuhudia wenzetu wanabatiza watoto wao.

 

Tukaomba kwa wazee wa kanisa bahati nzuri tumekubaliwa  mtoto wetu  kabatizwa  bila sisi wazazi wake kufanya maandalizi ya tukio hilo kubwa kiimani, mfano amekosa kumbukumbu ya picha kama tungelijua mapema tungekuambia wewe uje kumpiga picha”alimalizia kusema Baraka.

 

 Kwa upande wake Devary alisema”Kwanza nakushukuru sana kwa hili unalolifanya ya kuwaseme wasio nasauti Shemeji yangu ana Tv  kila siku wanasikilia  Mwamposa ambaye kwenye Tv yake amuweka mtaalamu wa Lugha za alama, wakiwa peke yao wanatoa sauti kwenye Tv wanamtazama mkalimali tu.”alisema

 

 Ifahamike Baraka anajimudu kidogo kifedha tunaamini kama angesikia tangazo hilo mapema angefanya maandalizi ya tukio hilo ikiwemo kuwaalika ndugu zake kutoka kwao Dodoma.

 

Ili kupata ufafanuzi wa jambo hili mtetezi wawanyonge aliwatafuta Viongozi wa dini Msaidizi wa Askofu Wilson Mafumbi  na Shehe Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Shehe Jafar Thinei ambao kwa pamoja wamefunguka mazito.

 

Majibu yao yatarukam hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.        

 

            


 

No comments:

Post a Comment

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...