Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, May 8, 2025

HABARI KALI YA KITAA,ASKOFU ASIGITISHWA MLEMAVU ‘KIZIWI’ KUTOAMBIWA TANGAZO LA UBATIZO KANISANI.


Baraka Simon na mkewe Blenda Martin pamoja na Mtoto wao Glory wakizungumza na Mwandishi wa habari hizi kabla kuelekea Kanisani.

 Ifahamike Simon na mkewe wote ni Viziwi lani Mungu ni Mkuu mtoto wao sio kiziwi.


 


 Kaimu Askofu ambaye kwa kanisa la Anglikana ni Mkuu wa wawachungaji wote wa kanisa hilo Dayosisi ya Morogoro Mchungaji Wilson Mafumbi akizungumza na Mwandishi wa habari hizi.


     Na Dustan Shekidele,Morogoro.

TAKRIBANI wiki tatu kipengele  pendwa cha habari kali ya kitaa hakikuwa hewani hii ni kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu, baada ya jambo kukaa sawa hatimaye kimejerea.

 

Baada ya kurejea Mwandishi wa mtandao huu alingia mtaani kusaka habari kali ya kitaa, na kubaini asilimia 90 ya madhehebu ya dini zote hayana wakalimali wa alama za vidole kwa waumini wao wenye ulemavu wa kusikia na kuongea’Viziwi’

 

Kufuatia hali hiyo  wenzetu hao ambao wanamtii Mwenyezi Mungu kwa kuhudhuria   lbada kusali na kuswali, kwa bahati mbaya sana wanapofika kwenye nyumba hizo za lbada hawasikii Mahubiri, Mawaidha na matangazo muhimu yanayotolewa na viongozi wao wa dini.

 

Hii ni kwa sababu asilimia 90 ya nyumba za lbada  zimejisahau kuwa kumbuka waumini wao hao wenye ulemavu wa kusikia’Viziwi’ ambao kimsingi nao wanahaki ya kusikia matangazo na mafundisho yanayotolewa na viongozi wao wa dini       

          MTETEZI WAWANYONGE

SIku zote Mwandishi wa habari hizi Dustan Shekidele kwenye kazi yake ya Uandishi wa habari ameamua kujitwisha mzigo mzito wa kuwatetea wanyonge sambamba na kuwaseme  wasio na sauti

 

 Binadamu wote nikiiwemo Mimi na  viongozi wa dini sote,tumeumbwa kusahau na kukosea, Ombi langu kwa Vingozi wote wa dini fanyeni tathmin kwenye nyumbani zenu za ibada mjue mnawaumini wangambi wenye ulemavu.

 

Ili mnapotoa huduma zenu za kiroho ziwafikie waumini  wote kwa usawa bila kulitenga kundi la waumini wenzetu wenye ulemavu,tukumbuke  ndugu zetu hao licha ya ulemavu wao bado wanajikongoja kuja kwenye nyumba za lbada kumuabudu Mungu wao huku baadhi ya watu wasio na ulemavu wakikwepa kuja  nyumba za lbada kwa Ubize wa kusaka pesa.

 Tusipowatengenezea wepesi kwenye nyumba hizo za lbada kwa kuwawekea ugumu wa kumuabudu Mungu wao wanaweza kujisikia vibaya hali itakayowakatisha tama ya kumuabudu Mungu wao.

Uchunguzi uliofanywa na Mtetezi wawangonge umebaini asilimia 90 za nyumba za lbada majengo yao wamejenga na kuweka njia Malumu ya waumini  wenye ulemavu wa Miguu ’ Viwete’.

.

Mtetezi wawanyonge anawaomba Viongozi wote wa dini kuweka wataalamu wa Lugha za Alama ili ndugu zetu Viziwi nao wasikie kila kitu.

Stori hii itaendelea baadae kwa uthibitisho wa Kiziwi mmoja kutoa ushuhuda kwa Mwandishi wa habari hizi  alivyopata kadhia ya Mwanae kubatizwa baada ya kutosikia Tangazo la Ubatizo licha yay eye kuwepo  kanisani.

Kufuatia malalamiko ya Muumini huyo Kiziwi Mwandishi wa habari hizi alimtafuta Askofu kujibu malalamiko hayo ya muumini wake, Askofu huyo amefunguka mazito juu ya tukio hilo endelea kuwa jirani na mtandao huu muda wote kwa muendelezo wa habari hii.

                    


No comments:

Post a Comment

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...