Huu ndio uwanja aliocheza Abdul ambao uko nje ya nyumba yao inayonekana kushoto yenye geti jeuzi
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Sehemu ya pili ya mahojiano Maalumu na Spear Mohamed Hamza ambaye ni baba mzazi wa beki kisiki wa ‘Wanafainali’ Simba Abdulrack Spear Mohamed Hamza.
Mahojiano haya jana yaliishia kwenye Kipengele cha kumuomba Spear kutoa historia fupi ya Maisha ya Mwanae alitoa historia hiyo kama ifuatavyo.
Spear. Awari ya toa kabla ya kutoa historia hiyo, tusimane dakika moja kumkumbuka Mama yake hayati Faudhia Ramadhan Mdeng’o aliyefariki dunia Aprili 11-2023 na kumzika Aprili 12 nyumbani kwao Magadu.
Nakumbuka Shekidele ulihudhuria mazishi hayo ya mpendwa mke wangu,barikiwa sana.
Spear aliendelea kutoa historia hiyo.
Abdulrazack. Ni mtoto wangu wa 3 kumzaa akitanguliwa na dada yake Neema na kaka yake Ramadhan,huku akiwa na wadogo zake wawili Natroli wa kiume na Nansi wakike.
Alimaliza darasa la saba shule ya Msingi Lenna iliyopo hapo mbele kama unaelekea Bigwa, alifaulu na kupangiwa kujiunga na Shule ya Sekondari Morogoro , huko alisoma mpaka kidato cha pili nikamuhamisha akajiunga na shule ya skondari Kingalu.
Akiwa shule alicheza Umiseta nakumbuka alikwenda Mwanza kwenye michuano hiyo ya Umiseta,toka yupo darasa la kwanza uwanja wake wa Mazoezi na mechi ni huo hapo nje
Niivyomuna Mwanangu anakipaji cha Soka niliamua kumpeleka Azam Academy, alikaa huko baadea akaenda Ndanda ya Mtwara iliyokuwa ikishiriki Ligi kuu” alisema Spear na kuongeza,
“Ndanda iliposhuka daraja akahamia Mbeya City, akatoka timu hiyo na kajiunga na Namungo,akakaa sana timu hiyo akajiunga na KMC Dar katoka KMC Kaludi tena Mbeya City
Baadae katoka Mbeya City kaenda Afrika Kusini kajiunga na timu ya Super Sport inayoshiriki Ligi kuu ya huko, alikaa Mwaka mmoja South Mwaka Jana karejea nyumbani na kujiunga na Simba
Nakumbuka aliporejea kabla ya kujiunga na Simba alicheza Ndondo Cup Saba Saba akiitumikia timu ya Damu Chafu nakumbuka Shekidele baada ya kumuna Abdularazack kule Saba saba ulinipigia Simu ukaniuliza Abdul ameludi lini kutoka South ukidai unamuna uwanjani Saba saba.
Mwisho wa historia yake Abdul ameoa ana mtoto mmoja anaitwa Sheina anasoma Cheke chea mkewe na Mwanae wako hapa kwangu kwenye nyumba hiyo ya pili”alimalizia kusema Spear
Baadae tutamalizia Stori hii kwa kuwasikia babu na bibi wa beki huyo wa Simba wazee hao nao wakitoa neno kwa mjukuu wao kuelekea Fainali hiyo’
No comments:
Post a Comment