Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, May 5, 2025

BABU NA BIBI WA BEKI KISIKI WA SIMBA WATOA NENO KWA MJUKUU WAO KUELEKEA FAINALI.



 


       Na Dustan Shekidele,Morogoro.

MZEE Mohamed Hamza Kondo na Mkewe Mama Dolli, wamempa Neno Mjukuu wao Abdulrazack Spear  Mohamed Hamza kueleka mchezo wa Fainali ya kombe la Shirikisho Barani Afrika ulipangwa kuchezwa nyumbani na Ugenini.

 Huku wanafainali Watoto wa Mama Samia ‘Simba’wakipata bahati ya kuanzia ugenini Mei 17 dhidi ya Rc Berkane ya Morocco na kumalizia nyumbani Mei 25.

 Kuelekea Fainali hiyo Mwishoni Mwa wiki Mwandishi wa habari hizi alitinga nyumbani kwa wazazi wa beki nyota wa Simba Abdulrazack Hamza,Mtaa wa Kigurunyembe Mzambarauni Kata ya Kilakala Mkoani hapa na kuzungumza na wazazi wa mchezo huyo ambao juzi na Jana Mtandao huu ulirusha mahojiano Maalumu ya baba mzazi wa mchezaji huyo Bw Spear Mohamaed Hamza ambaye alifunguka mengi kwenye mahojiano hayo.

Baada ya mahojiano hayo Mwana habari huyo alifanikiwa zungumza na babu na bibi wa mchezaji huyo ambao  wameamua kuishi hapo baada ya Mtoto wao Spear kupata mapigo makubwa mawili ya kupata ugonjwa wa Kiharusi’Stroke’.na kufiwa na mkewe.

Baada ya kupata maradhi hayo yanayohitaji usaidili wa hali ya juu,Mwaka uliofuata ndugu yetu huyo alipata mtihani mwingine wa kuondokewa na Mpendwa mkewake hayati Faudhia Ramadhan Mdeng’o aliyekuwa akimuuguza Mumewe kwa Upendo mkubwa Mwandishi wa habari hizi ni shahidi wa hilo.

Awari Wazee hao baada ya kumuona Mwandishi wa habari hizi Mama Dolli alisema.

“Hooo Shekidele habari za siku vipi Yule Mwanao  Tumaini’Mrembo’ uliyekuwa una mbeba kwenye Pikipiki kila siku kumpeleka shule ya Msingi Nguzo English Medium, yuko wapi siku hizi.?

Mwandishi.Tumaini kwa sasa ni mkubwa yuko Dar  anafanya kazi huko.

Ifahamike awari Mwandishi wa Mtandao huu alikuwa anaishi Masika katikati ya Mji wa Morogoro Mtaa wa Shamba jirani na Ukumbi wa Mango Garden, Mama Dolli na mumewe Wanaishi jirani na eneo hilo wakitenganishwa na Rell ya Kati wao wakiwa Mtaa wa Simu A kata ya Mji Mpya.

 Baada ya salamu hizo Wazee hao walitakiwa kutoa maoni yao kwa mjukuu wao kuelekea Fainali

“Kwanza tunamshukuru Mungu kumponya Mjukuu wetu, wewe shekidele ni shahidi hivi karibuni kwenye mechi kubwa Abdul alikuwa akiumia mara kwa mara kwa sasa tunashukuru ametengemaa.

Ushauri wetu kwake ajue hii mechi ni kubwa na yeye anacheza nafasi nyeti ya ulinzi hivyo ajitahidi kutofanya makosa yatakayo pelekea kuigharimu timu,sisi tunaendelea kumuombea dua yeye na timu yake ya Simba wafanye vizuri kwenye Fainali hiyo”alisema Mzee Kondo.

 

 

No comments:

Post a Comment

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...