Spear akizungumza na Mtandao huu jana asubuhi
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
SHABIKI ‘Lia lia’ wa Simba Spear Mohamed Hamza ambaye ni baba mzazi wa beki kisiki wa Simba Abdulrazack Spear Mohamed Hamza, amemfunda Mwanae kuelekea mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Renaissance Sportive de Berkane ya Nchini Morocco.
Kuelekea fainai hiyo Mwandishi wa habari hizi ambaye siku zote amekuwa mbunifu wa kusaka habari kali za chini ya kapeti, alifunga safari kwa usafiri wake wa Baiskeri hadi nyumbani wa Baba mzazi wa beki huyo wa Simba.
Akizungumza Kuelekea Fainali hiyo baba Abdulrazack alisema anaamini Simba watanyakua kombe hilo na yeye kuweka histori kwenye Maisha yake kwa mwanae kuchukua kombe la Afrika.
Fainali hiyo itapigwa kwa mikondo miwili mkondo wa kwanza wawakilishi hao wa Tanzania wanaoshika nafasi ya 4 kwa ubora wa vilabu barani Afrika ‘Mnyama’ Simba ataanzia ugenini Mei 17 atakapocheza na Waarabu hao.
Huku gemu ya mkondo wa pili ikipangwa kupigwa Mei 25 uwanja wa Mkapa uliopo Kata ya Mgurani Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam Tanzania.
Kwenye hili kama Mtanzania ninayeitakia mema timu ya nyumbani nawaambia Simba wamepata bahati ya kuanzia ugenini na kumalizia nyumbani, Wahenga wanasema siku zote ‘Tonge la mwisho ndio linalokomba mboga’.
Hivyo wanapaswa kufanya Ubaya Ubwela kwenye mchezo huo wa nyumbani kuhakikisha kombe hilo linabaki kwenye Ardh ya Tanzania, itakua aibu kubwa kombe hilo kutua Tanzania na kuondoka kwenda Rs Berkane Morocco.
Baada ya kufika nyumbani hapo Spear anayefahamiana vizuri na Mwandishi wa habari hizi, alimkaribisha kwa furaha, baada ya kukaribishwa Mwanahabari huyo alimjuia hali kisha kumpa Pole kwa kuugua.
Ifahamike ndugu yetu huyo ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Kigurunyembe Mzambarauni kata ya Kilakala, anasumbuliwa na Maradhi ya Miguu takribani miaka 3 baada ya kupata ugonjwa wa kiharusi ‘Stroke’
Mungu ni Mwema kwa sasa Spear anaendelea vizuri ingawa bado afya yake inaendelea kuimalika, baada ya kumjulia nahali sambamba na kumpa pole huku tukimuombea kwa Mwenyezi Mungu aendelea kumponya.
Tuliingia kwenye kipengele cha pili cha mahojiano ya Mwanae kua sehemu ya kuipeleka Simba Fainali na anamuhusia nini kwenye mchezo huo wa Fainali haya hapa majibu yake.
Spear. Shekidele asante sana kwa kuja kuniona na umekuwa Mwandishi wa kwanza kufanya mahojiano na mimi kuhusu Mwanangu kucheza Simba.
Mwandishi. Tuko pamoja Mkuu Vipi bado unaendelea na cheo chako cha uwenyekiti wa Mtaa huu?.
Spear. Hapana kutokana na haya Maradhi ya Miguu uchaguzi wa mwaka jana niliamua kupunzika nimemteua Mjumbe wangu kagombea nashukuru Mungu ameshinda Kwa Rehema za Mwenyezi Mungu afya yangu ikitengemaa uchaguzi ujazo nitareja kwenye kiti changu.
Mwandishi. Ok Mwenyezi Mungu atakuponya na utaendelea kuitumikia familia yako na wananchi wako wa Mtaa huu ambao ama kwa hakika najua wengi wao wanakupenda sana.
Awari ya yote kabla sijafika mbali ya mahojiano yetu kwa faida ya wasomaji wa Mtandao pendwa wa Shekidele tupe histori fupi ya Mwanao Abdulrazack.
Spear. Kwanza ifahamike watu wengi walijua Mwanangu ni Mzanzibar kutokana na hilo jina ukweli ni kwamba Abdulrazack ni Mluguru piwa kwa baba na Mama, Mimi baba yake ni Mluguru kutoka pale juu ya Milima ya Uluguru kijiji cha Mambate huku Mama Hayati Faudhia Ramadhan Mdeng’o ni Mluguru kutoka Kijiji cha Magadu jirani na kambi ya Jeshi ya Mzinga.
Historia yake fupi ni hii hapa…..
Mahojiano haya taendelea baadae kwa sehemu ya pili hivyo usikae mbali na Mtandao huu upate utamu wa mahojiano haya.
No comments:
Post a Comment