Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, May 27, 2025

KIJIWE NONGWA. UKIONA KAFUTA BANGO UJUMBE UMEFIKA

















 


Na Mpekunyuzi wa Mitandao Dunstan Shekidele.
 
Kama kawaida mtumishi wako, kila wiki naweka Bando linalonitembeza kwenye Mitandao ya Kijamii kukusanya jumbe mbali mbali.
 
Miongoni mwa jumbe hizo ni za Kuelimisha, Kukosoa na Maneno ya hekima yanayotukumbusha kuwa jirani na Mwenyezi MUNGU.
Tukutane Wiki Ijayo kwa mabango Mengine yenye Jumbe Moto Moto.

Monday, May 26, 2025

YAMETIMIA,KAZI INAENDELEA.




 


 Na Dustana Shekidele, Morogoro.

HATIMAYE Ujenzi wa daraja kubwa mto Morogoro eneo la Maghorofa ya Reli makutano ya Kata kubwa za Mji Mpya na Kichangani umeanza juzi.

 

Ikumbukwe siku za hivi karibuni Mtandao huu uliripo kwa undani ujenzi wa daraja hilo linalotajwa kuwa Mwarobani wa foleni za vyombo vya moto katikati ya Mji wa Morogoro.

 

Kwamba daraja hilo litakapokamilika watu watakao tokea barabarani ya Korogwe inayotoka Stend ya Msamvu kuelekea Kichangani, Kilakala.Kigurunyembe. Bigwa. ‘Kambi ya kulelea Wazee wasio jiweza ‘Funga Funga’.Gereza la Manispaa,  FFU Mkoa wa Morogoro’kikosi cha kutuliza ghasia cha Jeshi la Polisi’hawata lazimika kuingia katikati ya Mji badala yake watatumia daraja hilo wakiingilia Simba Oil kanisa la KKKT Usharika wa Mji Mpya wakivuka stend ya daladala ya Kaloleni Mji Mpya.

 

Jana Mwandishi wa Mtandao huu alishuhudia wanafunzi wa shule ya Msingi Kaloleni wakishuhudia Mtambo’Kijiko’ cha Mkandarasi kikiendelea na kazi ya ujenzi wa daraja hilo.

 

  Juhuzi za Mwandishi wa habari hizi za kutaka kuzungumza na Mkandarasi wa daraja hilo ziligonga Mwamba kwa sababu hakuwe eneo la tukio juhuzi hizo za kumsaka zinaendelea.

 Habari za awari zilizopatikana eneo la tukio  zinadai Mkandarasi huyo atakamilisha ujenzi wa daraja hilo ndani ya miezi minane’8’.

 Awari eneo hilo lilikuwa na daraja dogo lenye uwezo wa kupitisha, Pikipiki, Baiskeli na watembea kwa Miguu.  

Daraja hilo litakapokamilika kitachongwa kipande cha barabara kutoka barabara ya Lami ya Kichangani ikikatiza kando kando ya Uwanja wa Mazoezi wa timu ya Reli ya Morogoro, jirani na Shule ya Msingi Kaloleni ikifika kwenye daraja hilo inaungana na barabara ya kuelekea KKKT.

 

Kwa sasa kipande hicho cha upande wa pili wa kichangani hakina barabara, iliyopo ni ya watembea kwa miguu, Baiskeli na pikipiki.

Friday, May 23, 2025

SHULE YAVAMIWA NA MSITU, MKUU WA SHULE ADAI KIPAUMBELE CHAO NI TAALUMA.





 


   Na Dustan Shekidele,Morogoro. 

UKISTAAJABU ya Mussa hutoyaona ya firahuni,

Wakati  Shule ya Msingi Kaloleni ikijinadi hadharani kusimamia kwa vitendo‘Usafi, Nidhamu na utunzaji Mazingira, hali imekuwa tofauti mazingira ya shule hiyo ni machafu kufuatia kuvamiwa na msitu mkubwa uliozalishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.  

 

Kufuati hali hiyo Mtandao huu alimtafuta Mwalimu mkuu wa shule hiyo  Mikidadi Bakari alipulizwa alisema.

 

“Ni kweli kauli mbiu yetu ni hiyo angalia tumetunza mazingira kwa kupata miti eneo la shule, kweli kwa sasa kuna hivi vichaka mara nyingi huwa tunawaomba wafungwa wanakuja kutusaidia kufyeka, mvua vinakaribia kwisha nitaenda kuomba wafungwa waje kutufyekea” alisema Mwalimu huyo.

 

Alipoulizwa kwa nini wanafunzi hawafyeki ili hali huwa mnawaagiza wazazi  kununua mafagio na makwanja ya usafi?.

 

Mwalimu huyo alijibu. Kwetu sisi wanafunzi wako bize na masoma kwa sababu mwisho wa siku watapimwa kwa Taalumu na sio kwa kufyeka

 

Mwandishi. Nakumbuka wakati  nasoma kulikuwa na vipindi vya Masomo.Michezo na Utunzaji mazingira kwa maana ya kufagia na kufyeka,  tukipangiwa zamu chini ya usimamizi wa Mwalimu wa zamu.na Mwalimu Mkuu Mama Chausi.

 

Nakumbuka wakati nasoma hii miti ulikuwepo  kama mmepanda mingine basi imefichwa na huu msitu pia nakumbuka kulikuwa na bustani ‘Garden nzuri’ kwa sasa sioni nauona huu msitu  mkubwa ambao ni hatari kwa wanafunzi kwanza unaweza kutunza vitu hatarishi kama vile nyoka na Vibaka.

 

Mwalimu. Kweli unzi wenu na zetu ni tofauti na sasa mambo mengi yamebadilika yako kasi sana tunakimbizana na kasi hiyo hatuna muda wa kupoteza kimasoma.

 

Ifahamike Mwandishi wa habari hizi alisoma katika shule hiyo la kwanza mpaka la Saba na kwamba miaka ya hivi karibu Mwandishi wa habari hizi alikatiza kwenye shule hiyo na kushuhudia kibao cha shule hiyo kikiporomoka chini.

Kufuatia hali hiyo Mwanahabari huyo alijaribu kuzungumza na baadhi ya wanafunzi wenzie aliomaliza nao la saba akiwemo  Galula Jangalu ambaye kaka yake ni Kocha wa zamani wa timu ya Kagera Sugar Ally Jangalu.

 

Said Mtagwa ambaye naye kaka yake ni mchezaji nyota wa zamani hayati Jella Mtagwa.

 

 Msafiri Salehe Mdule ‘ambaye kwa sasa ni Kigogo wa Ardh Morogoro.

 

Wengine ni Adam Urasa Mfanyabiashara Maarufu Morogoro akimiliki nyumba za wageni Gest za Mangesho.

 Chiku Mwarami.  Doto na kulwa Sonny. Mawazo Adamu ambaye kwa sasa ni Mwalimu shule ya Msingi Kinole.

 Maneno Mtakahela Fundi Baskeli maeneo ya Mwembesongo. Subira Mkanile na Sawita, Kwa pamoja tulikubalia kufanya kitu kwenye shule kwa lengo la kurejesha fadhira ikiwemo kujenga kibao hicho cha shule.

Neno la kufurahisha  jana nilipofika nimeshuhudia kibao kipya kimejengwa kikiwa na kauli mbio hiyo ya ‘Usafi. Nidhamu na Utunzaji Mazingira’ ingawa nacho nilizingira na msitu.

 

Baada ya mahojiano na Mwalimu huyo nilijivua Uandishi wa habari nikaingia kwenye kipengele kilichonipeleka,nilimuahidi ‘Ticha’ huyo kwamba juhuzi za kuwaunganisha madent wenzangu hao zinaendelea hivyo mchakato  utakapokamilika tutafika shuleni hapo na kufanya jambo kwa maslahi mapana ya shule yetu.

 

Saturday, May 17, 2025

KANUNI KUMI ZA MAISHA YA NDOA. UKIZIZINGATIA NDOA YAKO ITADUMU.


 


1.    USIJIHUSISHE NA HUSIANO MENGINE KWA LENGO LA KUEPUSHA MIGOGO ISIYO YA LAZIMA ILI KUENDELEA KULINDA  MAHUSIANO YAKO NA MWENZI WAKO: Pasitokee MTU mwingine (wa jinsia yeyote) ambaye atakuwa na umuhimu wa juu zaidi kuliko mwenzi wako.

 

 

2.    USIMLINGANISHE AU KUMSHINDANISHA MWENZI WAKO NA MTU MWINGINE: Kumbuka kila mtu yupo tofauti. Tumia hekima kumfanya mwenzi wako awe bora zaidi pasipo kumfanya ajisikie  hafai au hana viwango unavyotaka wewe.Kuwa mbunifu kila siku kwenye mahusiano yako ili yawe mapya siku zote.

 

 

3.    USITUMIE “TENDO LA NDOA” KAMA FIMBO YA KUMWADHIBU MWENZI WAKO. Hata kama mmepishana misimamo, kumbuka “Tendo la Ndoa” ni haki ya msingi ya kila mwanandoa. Ndio kiini cha nyinyi kuunganishwa kuwa mwili mmoja,kama mmekuwa mwili mmoja hakuna binadamu yoyote anaye chukia sehemu ya kiungo chake mwilini.

 

 

4.    USIISHI MAISHA YA SIRI KWA MWENZI WAKO. Fanya jitihada za makusudi kuvunja kila tabia ya usiri ambayo itasababisha kila mmoja aishi maisha yake binafsi.kuwa muwazi kwa kila kitu hata ikitokea mwezi wako hayupo uwe na uwezi wa kufungua pini [Namba za Siri] kama vile Bank na kwenye mitandao ya simu.

 

5.    USIJILAUMU KUINGIA KWENYE NDOA AU KUMWONYESHA MWENZI WAKO KWAMBA UNAWEZA PATA MBADALA WAKE WAKATI WOWOTE. Hata kama unahisi “ulikosea kumpata” hayari huo ni msalaba wako ubebe huku ukifanya wajibu wa kuiboresha hiyo ndoa hakuna kinachoshindikana hapa chini ya Juwa. Kumbuka UPENDO una nguvu kuliko MAUTI.

 

 

 

6.    USIRUHUSU KAZI AU MAJUKUMU YAKO YAIDHOOFISHE NDOA YAKO: Pamoja na majukumu mengi uliyonayo, hakikisha umuhimu wa ndoa yako unabaki palepale.usiwe bize na majukumu kiasi cha kuisahau familia.

 

7.    USIWE MBINAFSI.Usipendelee mambo yako tu au ndugu zako tu; bali kumbuka pia mwenzi wako naye ana ndugu zake na anamambo yake.hivyo kila jambo unalofanya liwe la uwasa.

 

 

8. USIWE MWEPESI KUSAMBAZA MAMBO YENU YA NDANI KWA KILA MTU: Ndoa ni taasisi yenye kanuni na taratibu zake; mojawapo ya kanuni hizo ni “utunzaji wa mambo nyeti” (Confidentiality). Uwe makini unamwambia nani kitu gani. Natambua kwenye ndoa sio pemboni kwamba kila siku utakuw ana furaha na amani ya Moyo, hapa haiku hivyo kuna siku mtakwazana mtachukizani. Ikitokea hali hiyo ukukwaluzana pakubwa kiasi cha kutishia uhai wa ndoa yenu, hivyo kuhitaji usaidizi wa watu wengine.

Kuna watu sahihi wa kuwashirikisha ambao ni wazazi, Wasimamizi wenu wa ndoa{Mashahidi wa ndoa yenu] huko kote ikishindanani basi fikeni kwa viongozi wa dini waliofungisha ndao yenu ambao wana kanuni za mafundisho ya ndoa.

 

8.    USIJIDANGANYE KWAMBA KUNA MTU MWINGINE ANAKUPENDA NA KUKUJALI ZAIDI YA MUME/MKE WAKO: Kumbuka kuna watu wataonyesha wanakujali sana kwa sababu sasa upo kwenye ndoa; siku ukitoka hutaamini kama ndio wale!! watakupita kwa kasi ya ‘SGR’ huku wakikufungia vioo usiwaone.

 

 

10. USISAHAU KIAPO CHA NDOA NI KIAPO CHA DAMU… NI KIAPO CHA MAISHA: Usiruhusu mawazo ya kutengana au kuachana yawe RAHISI na MEPESI sana ndani ya kichwa na moyo wako. Mara zote katika changamoto jikumbushe KIAPO CHA NDOA… “Nitakuwa nawe katika hali zote…!!” kubwa zaidi ni kusameahana pale mnapokoseana na kuoweka visasi vya kijinga moyoni ukiamua kusamehe same kweli usihifadhi visasi moyoni.

NYONGEZA.

OMBEA ondea ndoa yako kila mara na ikitoea mtikisiko basi Paleka shida zako kwa MUNGU kabla hujazipeleka kwa Mashoga zako au Marafiki zako hao hawata kusaidia chochote zaidi ya kukutangaza.

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...