Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, April 7, 2025

KARUME DAY, MH DIWANI ATOA SADAKA KWA NDEGE NJIWA.

                                    Ramadhan Rajabu
                                                     Nassoro Hamoud' Mpemba'

                                Mhe Hassan Malingo

 


       Na Dustan Shekidele Morogoro.

AMANI ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi wadau wote wa Mtandao Pendwa wa Shekidele, ama baada ya salamu, naomba radhi kwa kutokuwa hewani kwa takribani siku 10.

Hii ni baada ya kuwa likizo iliyonifanya niende sehemu kupunzisha akili, nimerejea Leo kuendeleza kazi ya kuwapa habari Moto Moto za chini ya Kapete hivyo usicheze mbali na Mtandao huu kuna habari kali.

Nimeanza Kazi Leo Jumatatu ya April 7 siku ambayo Taifa la Tanzania Linaadhimisha kumbuziki ya Kifo cha Mpendwa wetu hayati Abeid Aman Karume Rais wa kwanza wa Zanzibar.

Hayati Karume aliuwawa na watu wasiojulikana Apeil 7 -1972 hivyo Leo April 7- 2025 ametimiza miaka 53 ya kifo chake.

Kama kawaida Mwandishi wa Mtandao huu ambaye siku zote anatumia ubunifu mkubwa kusaka habari za tofauti, Leo baada ya kuanza kazi aliamua kwenda Mtaa wa Karume uiopo kata ya Mji Mkuu Mkoani hapa kwa lengo la kuzungumza na wananchi wa Mtaa huo uliobeba jina la Karume.

Nilipofika kwenye mtaa huo moja kwa moja nilitinga kwenye Mgahawa wa Mpemba ambao ni maarufu mkoani hapa kwa kuuza Al- Kasusu. Karanga, Maandazi Kacholi Asari na Juice ya Bungo.

Mtandao huu ulipofika kwenye Mgahawa huo ambao  upojirani na Msikiti wa Karume alimshuhudia diwani wa Kata hiyo Mhe Hassan Malingo[aliyechuchumaa] akitoa zawadi ya Karanga mbichi kwa kundi kubwa la Njiwa waliokuwa wakimpanda mikononi mabegani na kichwani wakigombea zawadi hiyo ya chakula.

Mhe huyo lifanya hivyo kwa kushirikiana na Mmiliki wa Mgahawa huo  Mpemba Nassoro Humoud.

Akihojiwa na Mtandao huu Mhe Malingo alisema”Leo ni karume Day kwenye kata yangu ya Mji Mkuu inamitaa miwili yenye majina ya hayati karume,kuna Mtaa wa Aman ule pale juu na hapa tulipo ni Mtaa wa Karume.

Hivyo muda huu nimetoka kuswali nimepita hapa kunywa Kasusu nimeona ninunue karanga nitoe sadaka kwa hawa Njiwa shekidele na wewe karibu unywe kasusu”alisema Mhe Maingo

lfahamike Mhe Malingo kabla ya kuuvaa udiwani wa kata hiyo iliyopo katikati ya Mji alikuwa Katibu Mkuu wa timu ya Moro United  “Chelsea ya Bongo”iliyomiikiwa na tajiri wa mafuta mwana Morogoro Mwarabu Merey Balhabou.

Wachunguzi wa Mambo wanadai kata hiyo  ndio kati tajiri kati ya kata 29 za Jimbo la Morogoro,ikifuatiwa na kata ya Mafisa yenye viwanda vingi na Stend ya Mabasi ya Msamvu.

 Kwa upande wake Mmiliki wa Mgahawa huo Hamoud alisema Njiwa hao sio wake ni wamajirani zake, wamezowe kufika eneo hilo kila siku kwa sababu huwapa chakula kama sehemu ya sadaka yake kwa viumbe hao.

                 HISTORIA FUPI YA NJIWA

Miaka ya nyumba Mungu alichukizwa na  vitendo viovu vilivyofanywa na binadamu hapa ulimwenguni kabla ya kuuangamiza ulimwengu kwa maji alimwambia Nuhu atengebeze safina na wale watakatifu waliingia kwenye hiyo safina.

Baada ya safina hilo kutengemaa na watu wake safi kuingia ndani ,Mungu alionyesha uunguwake kwa watenda dhambi alishusha Upepo mkali nayo maji ya Gharika ya maji ilishuka kutoka milimani,kwa siku Arobaini Mfurulizo Nuhu na wenzie walielea kwenye safina ‘Mwanzo 7-11-13’

Baada ya siku kadhaa kupita watu hao walimtuma ndege Kunguru kwa sababu anauwezo wa kuruka  akaangalie kama maji yamekauka ili watoke kwenye safina.

Kunguru alipofika na kukuta maji yamekauna huku eneo hilo likitapakaa mizoga ya wanyama na watu Mwamba huyo aliamua kula mizogo hiyo na kusahau kurejea majibu kwa aliyemtuma.

Watu hao baada ya kuona kunguru harudi wakaamua kumtua Njiwa ambaye alikuwa Mwaminifu alikuta maji yamekauka, hivyo hakuwa na tama ya kula mizoga alichofanya alitua chini na kuchukua jani kavu mdomoni fasta akareja kwa aliyemtuma na mueleza kwamba huko mambo ni swali maji yamekauka kiasi cha kutua chini na kubena kijiti.

Kwa histori hiyo ndio maana mpaka Leo Njiwa anapotaka kutaga anajenga kiota chake kwa kuokota vijiti vikavu, huku Kunguru akiendelea kuwa kero mtaani kwa kukwapua mizoga, ukiacha wazi sinia lako la samaki utakuta leupe.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

KIJIWE NONGWA. UKIONA KAFUTA BANGO UJUMBE UMEFIKA

  Na Mpekunyuzi wa Mitandao Dunstan Shekidele.   Kama kawaida mtumishi wako, kila wiki naweka Bando linalonitembeza kwenye Mitandao ya Kijam...