Na Dustan Shekidele.
WASHIKA Bunduki wa Jiji la Maraha la London nchini England Arsenal usiku wa leo imeishangaza dunia baada ya kuwakanda Mabingwa wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya’UEFA Champion League’ Real Madrid ya Hispania kwa kuinyuka bao 3-0.
Mabao yote yamefungwa kipindi cha pili na Mwamba Rice aliyefunga mabao 2 kwa mikwaju ya faulo nje ya 18.
Bao la kwanza akifunga dakika 58 na la pili akifunga kwa style hiyo hiyo dakika 70, huku bao la 3 likifungwa na Merino dakika ya 75
Gemu hiyo ya mkondo wa kwanza imepigwa majira ya saa 4 usiku na kutamatika Muda huu saa 6 usiku kwenye Uwanja wa Emirates unaomilikiwa na Arsenal, mechi ya maludiano inatarajiwa kupigwa wiki ijayo Jijini Madrid Hispania kwenye dimba la Santiago Bernabeo.
Real ambao ni mabinga watetezi wa kombe hilo ili wafanikiwa kuvuka Nusu fainali na kutetea ubingwa wao wanapaswa kuifunga Arsenal bao 4-0.
Kinyume na hapo watakuwa wamevuliwa ubingwa na chama hilo la Wana Arsenal ambao kwa sasa ni moto wa kuotea mbali hapa duniani,tusubiri tuona matokeo ya gemu ya Mkondo wa pili.
Pichani Mwandishi wa habari hizi ambaye ni shabiki lia lia wa Arsenal akiwa amejifunika shuka la timu hiyo.
No comments:
Post a Comment