.......Hata anatafakari alipokaribia kwenye jeneza
Akiangua kilio
......Akianguka chini kaba ya kumaliza mzunguko wa jenzeza
...Akiingizwa ndani
......Watu wakimpa huduma ya kwanza ya kumpepea kuia Kendi akimtazama Mama yake kwa uchungu .
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
MWAMUZI wa kike Mkoani Morogoro wa Daraja la Kwanza Happinessi Tamba, Mwishoni mwa wiki akiwa na ujauzito mkubwa ameanguka na kupoteza fahamu wakati akimuaga mzazi mwenzake Marehemu Victor Reuben Ngome Maarufu Mswaki ambaye pia ni mchezaji nyota wa ligi daraja la kwanza Tanzania Bara.
Mwandishi wa habari hizi aliyekuwepo Msibani hapo Mtaa wa Bigwa Kisiwa kata ya Kilakala Manispaa ya Morogoro alimshuhudia Happy akisaidiwa kupita kwenye jeneza lililobeba mwili wa mpendwa Mzazi mwenzake huyo aliyezaa naye mtoto mmoja wa kiume anayeitw a Kendi.
Alipofika kwenye jeneza hilo na kumuona Mzazi mwenzake huyo Happy alianguka chini akifikia Tumbo na kupoteza fahamu,alinyanyuliwa na kundi la watu na kuingizwa ndani ambako alilazwa kwenye mkeka akazungukwa na kundi hilo la watu waliompa huduma ya kwanza ya kumpepea na nguo.
lnasigitisha sana wakati watu hao wakiendelea na huduma hiyo Mtoto Kendi pichani kulia aliangua kilio aliposhuhudia mpendwa Mama yake amelala chini na kupoteza fahamu
Kwa Rehema za Mwenyezi Mungu baada ya dakika kama 20 hivi Happy alizinguka na kurejea kwenye hali yake ya kawaida.
Kufuatia tukio hilo baba mzazi wa Happy Mzee Tamba kwa kushirikiana na familia ya Marehemu Mswaki walikubaliana kwa kauli Moja kwamba kutokana na hali ya Happy asisafiri kwenda Tanga Kumzika Mzazi mwenzake jambo hilo liliungwa mkono na waombolezaji wengi ambao baadhi yao walishauri hata kwenye tukio la kuaga hasingeruhusiwa kufanya hivyo kutokana na hali yake hiyo.
lfahamike refa huyo maarufu mkoani Morogoro Happiness Tamba baba yake mdogo ni Afande John Tamba anayeifundisha timu ya Polisi Tanzania.
Hayati Mswaki alikuwa Mdau mkubwa wa Mtandao wa Shekidele baadae Mtandao huu utarusha picha kibao za Mswaki akiwa kwenye matukio mbali mbali uwanjani na kile alichokisema mchungaji kuhusiana na kifo cha Mswaki, hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao Pendwa wa Shekidele muda wote kwa habaqri za chini ya Kapeti ambazo huwezi kuzikuta popote.
No comments:
Post a Comment