KUMBUKIZI.
VIGOGO Morogoro wahudhuria Dabi ya Masoko iliyopigwa uwanja wa CCM Jamhuri.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood [Kushoto] ambaye pia ni Mmiliki wa Mabasi ya Abood,akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania’TFF’ Wales Karia.
Hii ni Mwaka 2017 walipohudhuria Dabi ya timu zenye upinzani Mkali Mawenzi Market inayomilikiwa na wafanyabiashara wa Soko la Matunda la Mawenzi na Saba saba United inayomilikiwa na wafanyabiashara wa Mnada wa Jumapili soko la Saba saba.
Mwaka huo timu hizo zenye nguvu kubwa ya pesa zilikuwa zikishiriki ligi daraja la pili Taifa, kwa sasa timu hizo zimekufa hazipotena kwenye ulimwengu wa Soka.
Ikumbukwe utawara wa awamu ya Nne Karia alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro,na kwamba utawara wa awamu ya Tano ulipoingia madarakani ulimuondoa kwenye nafasi hiyo. Picha na Dunstan Shekidele,Morogoro.
No comments:
Post a Comment