Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, February 4, 2025

KUMBE MTAALAM ANAUWEZO WA KUPANDA MIGOMBA TU UTAALAM WA KUNG’OA HANA.






 


                                       Na Dustan Shekidele, Morogoro.
SIRI imefichuka kumbe yule ‘Mwamba’ Salumu Mwapu Mwinyikufa Mzaramu kutoka Mwanalumango Yombo Lukinga ‘Baba Rama’ anautaalam wa kupanda migomba tu utaalam wa kuingoa hana.
 
Juzi Mtandao huu ulirusha picha na habari zinazomuonyesha Mtaalam huyo akipanda miche ya Migomba kwa utaalam wa hali ya juu kiasi cha kuwavutia wengi.
 
Mzaramo huyo aliyerowea Mji Kasoro Bahari’Morogoro’ baada ya kuchimba shimo kwa ustadi mkubwa aling’oa miche ya migomba iliyopandwa nyuma kwa lengo ya kuendelea kupanda mingine eneo hilo.
 
Mtaalam huyo aling’oa miche 3 na kwamba baada ya kuong’oa aliipanda kwenye mashimo hayo.
 
Balaa kubwa Siku hiyo hiyo usiku mvua iliyoambatana na upepo ilinyesha mkoani Morogoro .
 
Kulipo kucha Mwandishi wa Mtandao huu alishuhudia mgomba uliobeba mkungu mkubwa wa ndizi ukianguka chini.
 
Uchunguzi wa awari uliofanywa na Mwandishi wa habari hizi umebaini Kilichosababisha mgomba huo kuanguka ni baada ya baba Rama kuchimba shimo na kukata sehemu kubwa ya mizizi ya mgomba huo wakati aking’oa’miche’ watoto wa mgomba huo aliyochomoza sehemu kubwa ya mzunguko wa Mgomba huo.
Baada ya kuona majanga hayo Mwanahabari huyo alimtwangia simu Mzaramu huyo na kumjuza madhara hayo yaliyosababisha hasara majibu yake haya hapa.
 
“Nisamehe bure Shekidele kwenye vibarua ninavyofanya kwenye mabanda ya maonyesha Nane nane nimepata utaalam wa kupanda migoma lakini utaalam ya kung’oa miche Mabosi wangu hawakunipa.
 
Hii ni kwa sababu mara nyingi miche ya Migomba inaletwa kwenye maonyesho ikiwa tayari imeng’olewa huko mashambani”alisema Baba Rama na kuongeza.
 
“Ni kweli kwa jinsi nilivyochimba chimo kubwa wakati naing’oa ile miche lazima ule mgomba ulikuwa umebeba mkungu mkubwa uangushwe na ule upepo wa jana usiku.ila nimepata somo Mungu akijaria maonyesho ya Mwaka huu nitawaambia wataam wangu wanifundishe jinsi ya kungoa miche bila kuathiri mgomba uliobeba Ndizi”alimalizia kusema Mwinyikufa.
 
Mwandishi wa Mtandao huu alimtangazia msamaha wa bure Mzaramo huyo akimueleza kwamba hizo ni moja ya changamoto za kazi

No comments:

Post a Comment

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...