Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, February 11, 2025

HABARI KALI YA KITAA. KIFO CHA AFANDE MAJIRANI WAMTUPIA LAWAMA MKE.

Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa River Side Hashimu Bito akizungumza  na Mtandao huu

 Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa River Side Fatuma Abdallah Mmelo akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu

 

    Na Dustan Shekidele,Morogoro.

KAMA kawaida  kila wiki Mwandishi wa Mtandao huu huingia mtaani kusaka habari kali ya kitaa na kuirusha hewani kila Jumanne kwenye Mtandao Pendwa wa shekidele unaofuatiliwa na watu wengi pande zote za Dunia.

Wiki iliyopita Mwandishi wa habari hizi alipigiwa simu na mkazi mmoja wa Mtaa wa River Side Kata ya Mwembesongo Mkoani hapa akisema.

”Shekidele njoo uchukue habari ya mke kudaiwa kuchangia kifo cha mumewake”.

Alioulizwa kwa nini anasema mke huyo kachangia kifo hicho? alijibu.

“Huyu Mzee alikuwa anaumwa ugonjwa wa Tezi dume wanae wanaoishi Dar wametuma laki 5  akafanyiwe ubasuaji bibi anadaiwa kula  pesa hiyo na kuendelea kumfungia mgonjwa ndani hadi aliofariki dunia juzi jumatano”alisema jirani huyo.

 

Wakati Mwandishi huyo anapokea taarifa hiyo alikuwa safarini Mikumi aliporejea jumapili alitinga  mtaani hapo kufuatilia habari hiyo nzito.

Alipofika kwenye nyumbani hiyo aliyokuwa amepanga marehemu  alimkuta mama mmoja akipanga  bidhaa kwenye Genge lililopo nje ya nyumba hiyo.

Alipoulizwa kuhusiana na taarifa hizo Mama huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema.

“Ni kweli taarifa hizo zinaukweli kwa asilimia 80 mzee alikuwa anaumwa takribani mwezi mzima kapiga simu Dar kuwajulisha ndugu zake wakatuma Pesa ya matibabu laki 5 ilipoingia kwenye simu ya bibi kapiga kimya hakumjulisha mumewe.

Juzi jumanne jioni masikini ya Mungu tumemsikia mzee alilalamika maumvu makali baadae kamuliza mkewe hao watoto hawajatuma hizo pesa za matibabu?bibi kamjibu kwamba wametuma lakini zimeibiwa Mzee kaanza kufoka ‘zitaibiwaje na kwanini hukuniambia kama zimetumwa? zogo  liliendelea  siku iliyofuata  jumatano Mzee wawatu amefariki”alisema Mama huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Alipoulizwa bibi huyo amekwenda wapi Mama huyo alisema.

” Kwanza niwe mkweli sisi kwenye nyumba hii wengi hatuongea naye aliya kwamba tunaishi nyumba mmoja binafsi nata namba yake ya simu sina.

Ninachoweza kusema Kwenye kikao cha familia kilichoketi jana bibi katakiwa kutaja mali alichochuma na mumewe  kadai mbele ya kikao kwamba marehemu hana mali yoyote zaidi ya nguo zake tu na baiskeri, jambo hilo liliwakera ndugu hao wa marehemu ambao wanajua mzee wao anamali ikiwemo nyumba.

Wakamuliza je ile nyumba bibi kasema nyumba ile kajenga yeye mumewe hausiki,  ndugu kama wamemsusia flani wakamuambia sana kama hiyo nyumba mzee hajahusika chochote  baki nayo, wakamtoa nje wakachukua vitu vyote vya ndani wakaludisha chumba kwa mwenye nyumba wakatawanyika, hatujuia huyo bibi alikoenda ” amemalizai kusema  shuhuda huyo.

Mwandishi wa habari hizi alimtafuta mmoja wanafamilia aliyeshiriki kikao hicho aliyekubari kutoa habari kwa sharti la kutotajwa jina lake popote.

“Shekidele mimi ni ndugu upande wa yule bibi lakini kwa sababu ninahofu ya Mungu kwenye kikao kile nilikuwa upande wa familia ya marehemu.

Kiukweli bibi ni msheni kwa sababu mumewe kakata kauli hawezi kujitetea  anatumia nafsi hiyo kudhurumu haki zake.

Kwenye kikao cha jana ndugu wa marehemu walikuwa na nia njema wamemtaka  ataje mali walizochuma na mumewe ufanyike mgawanyo wa haki, chaajabu Yule bibi kasema marehemu hakuwa na mali yoyote ili hali kama wafamilia wanajua wawili hao wamejenga nyumba iko Kasanga”alisema Jamaa huyo na kuongeza.

Mimi najua wawili hao wameishi pamoja toka mwaka 80 Mzee alikuwa Askari akilinda holeli ile ya kitalii ya Oasisi kajibana yeye na mkewe wamenunua kiwanja Kasanga alivyostaafu kamalizia nyumbani na malengo yao januari ya mwaka huu mpya wahamie kwenye nyumbani yao lakini wameshindwa kufanya hivyo kwa sababu choo kilikuwa bado hakijakamilika hivyo lengo lao mwisho wa mwezi huu kodi yao ikisha kwenye nyumba ile wahamike kwao kwa bahari mbaya mzee amefariki kabla ya kuingia kwenye nyumba yake”alimalizia kusema mwanafamilia huyo.

Alipoulizwa wazee hao wamejaliwa kuzaa watoto wangapi alijibu.

“Hawakujaliwa kuzaa ila marehemu kabla ya kuishi na huyu mama alikuwa na mahusiano mengine huko alizaa watoto wawili wakike na kiume .

 Mtoto wake wa kike alifariki dunia na kuacha  watoto wawili  mmoja  ni Mwanajeshi aliyetuma laki 4 za kumpeleka babu yake hospitali kufanyia upasuaji wa tezi dume.

Chaajabu pesa hizo huyu bibi hakuziwasilisha kwa mgonjwa sijui kazipeleka wapi, hilo lano mjukuu huyo Mjeshi [anamtaja jina]  alimchukiza sana ”alisema Mwanafamilia huyo ambaye ni shabiki kindaki ndani wa Simba.

Aliulizwa  huyo bibi anawatoto wangapi? Alijibu. “ Maisha yake yote hajabahatika kupata mtoto nao watoto wanaomkingia kifua ni watoto wa wadogo zake na kaka zake”.

  Mwandishi wa habari hizi alimtafuta  bibi huyo ambaye ni maafuru mtaani hapo kwa jina la bibi Ndizi kwa njia ya simu ili kusikia kauli yake juu ya shutuma hizo zinazomkabili namba hiyo haipatikani kwa siku 2 mfurulizo.

Kwa sababu  hajapatikana  kwa kuzingatia kanuni za Undishi wa habari Mtandao huu  ameradhimika kuhifadhi jina lake na jina la marehemu hadi hapo atakapopatikana kujibu madai hayo  juhudi za kumtafuta  zinaendelea.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huu Hashimu Bito amethibitisha kutokea kwa tukio hilo

”Ni kweli tukio hilo limetokea  niseme tu kwamba Mzee huyo [anamtaja jina] alifariki Jumatano tumemzika ljumaa makaburi ya Kolla.

Jana jumamosi Mjumbe wangu Mama Juma ananipa taarifa kwamba kunamzozo kwenye nyumba ya marehemu nikashangaa mtu tumzika jana leo mzozo  nikamwambia aende eneo la tukio, hivyo kwa habari zaidi za vulugu hizo za mke  na ndugu wa marehemu nenda kwa Mjumbe wangu Mama juma atakuba habari kamili”amesema Bito pichani mwenye nguo ya kijani.

Kwa upande wake mjumbe huyo aliyejitambulisha kwa jina la Fatuma Abdallah Mmelo Maarufu Mama Juma alisema.

”Ni kweli jana nilikuwepo  kwenye vulugu niwe mkweli Yule mama alichofanya sio sawa kama ningejua mapema mabaya aliyomfanyia marehemu hata ile Rambirambi ya mtaa elfu 40  nisingemkabidhi.

Naamini hata wale watu la kanisa analosali la TAG ‘Bethel Revival Temple’ Mwembesongo wangesikia vitendo alivyomfanyia mume wake wasingempa Rambirambi ya laki Moja na Arobaini ”alisema Mjumbe huyo pichani aliyejifunika mtandio kichwani.

 

 

No comments:

Post a Comment

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...