Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, February 1, 2025

MZARAMU MTAALAMU W AKUPANDA MIGOMBA.






 


    Na Dustan Shekidele,Morogoro.

MTAALAMU wa kupanda migomba mkoa wa Morogoro afunguka mazito namna ya kupanda migomba inayozaa ndizi kubwa.

Jamaa huyo aliyejitambulisha kwa jina la Baba Ramadhani Maarufu Mzaramu wa Dar es salaam aliyerowea Morogoro anautaaramu mkubwa wa kupanda Migomba.

Baba Rama alipanda  Mgomba nyumbani kwa Mwandishi wa habari ambaye alivuna mikungu mikubwa ya Ndizi kama inavyoonekana pichani  akienda kuuza mmoja wa Mikungu hiyo. Alipotakiwa kueleza namna ya kupanda miche hiyo ya Migomba baba Rama alisema.

” Unachimba shimo la urefu wa futi 3 katikati ya shimo hilo unachimba kimfereji mfano wa kimwanandani  unaweka mbole eneo hilo kasha unaweka mche wa Mgomba kisha unafugia na ugondo shimo hilo urefu wa fundi moja kasha unamwagia maji ndoo moja lita 20 asubuhi na jioni kwa muda wa siku 3.

Baada ya hapo mgomba huo utakuwa na kuzaa watoto kwenye mzunguko wa shimo hilo ukianza kuzaa mkungu wa ndizi unakuwa mkubwa kama huu”alisema baba Rama ambaye gharama zake kupanda mgomba mmoja ni shilingi elfu 3. Alipoulizwa utaalamu huo ameupatawapi alijibu.

”Utaalamu huu nimeupata  Kwenye maonyesha ya Nane nane huwa nafanya vibarua kwenye mabanda wakati wa maonyesha ya wakulima Nane nane Kanda ya Mashariki yanayofanyika kila Mwaka hapa Morogoro.

Hata hivyo Mtaalamu huyo kwenye kazi hiyo amemtia shoti Mwandishi wa habari hizi shoti gani hiyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote ushuhudie hasara hiyo.

 

No comments:

Post a Comment

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...