Na Dustan Shekidele,Morogoro.
IFAHAMIKE toka Tanzania ipate uhuru Mwaka 61 kata Kongwe ya Chamwino iliyopo katikati ya Manispaa ya Morogoro haijawahi kuwa na barabara ya Lami.
Juzi kwa mara ya kwanza chini ya Uongozi wa Rais Mh Dkt Samia Suluhu Hassan’SSH’ Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia moja ya barabara kubwa za kata hiyo ikiwa kwenye ukarabara wa kuweka Lami.
Mwanahabari huyo alimshuhudia Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Dkt Abdulaziz Mohamed Abood akikagua ujezi wa barabara hiyo inayotoka lringa Road mpakani mwa kata hiyo na Kata ya Kiwanja cha Ndege eneo la Kwa Jeta kuelekea kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania I.G.P Mstaafu Alhj Omar ldd Mahita.
Mhe Abood alisema barabara hiyo yenye urefu wa Kilometa 2.1 awamu ya kwanza itawekwa Lami mita 900 kwa maana ya kutoka kwa Jeta mpaka Transphoma na awamu ya pili watamalizia kilometa 1.2
“Kwetu sisi wakazi wa Kata ya Chamwino haya wanayotufanyia Rais Samia na Mbunge wetu Abood ni kama ndoto kwetu, kwenye kata yetu hatujawahi kuwa na barabara hata moja ya Lami toka duniani hii imeubwa” amesema Zumbe Cool ambaye ni bingwa za zamani wakucheza Disco Mkoa wa Morogoro.
Kwa sasa Zumbe ni Dj Maarufu Kata hiyo ya Chamwino akimiliki seti mbili za vyombo vya Muziki, na kwamba Vidogolo vingi vya Chamwino wananchi wanakodi Muziki kwa Staa huyo ambaye pia ni Fundi Baskeri mtaa wa Karume Kata ya Mji Mkuu.
Jimbo la Morogoro Mjini lina kata 29 na Mitaa 294 huku kata ya Chamwino ikiwa ni Moja ya Kata kongwe kwenye Jimbo hilo linaloongozwa na kipenzi cha wana Morogoro Tajiri Mh Aziz Abood.
No comments:
Post a Comment