Baba mzazi wa Dick akihojiwa na Mtandao huu jana mchana.
Dick akiwa na kombe baada ya timu yake ya Moro Kids kutwaa ubigwa wa Ligi ya Vijana uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Gazeti la Msimbazi liripoti tetesi za beki kisiki wa Yanga Dickson Nickson Job kutakiwa na Simba kwenye usajiri wa Dirisha kubwa unaotarajiwa kufanyika baada ya ligi kuu kutamatika mwezi wa tano mwaka huu.
Baada ya kusoma habari hiyo jana Mwandishi wa habari hizi jana hiyo hiyo aliwatafuta wazazi wa mchezaji huyo kwa lengo la kusikia ushauri wao kwa kijana wao.
HUYU HAPA BABA MZAZI. Akizungumza na Mtandao huu Nickson Job Mwakisesile ‘Mnyambara’ kutoka Kyela Mbeya alisema.
“Ni kweli mkataba wa Yanga na Mwanangu unakaribia kwisha, kabra sijajibu swali lako shekidele ufahamu kwamba mimi na mama yake wote ni mashabiki lia lia wa Yanga ukitoka hapa nenda pale saba saba kwenye duka lake ukazungumze naye.
Kwangu Mimi kwenye shwara hili ushauri wangu unamajibu mawili Mosi angalie upanda wenye masrahi mazuri,Pili angalie sehemu ambayo anaaminika na kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara hivyo kama Yanga watamboreshea masrahi kwenye mtakaba wake mpya abaki Yanga na hili nitamwambia na Meneja wake George Mwakisesile ambaye ni Mdogo wangu ”alisema mzazi huyo Maarufu kwa jina la shukuru akiwa kwenye duka lake kubwa la Spea za Pikipiki lililopo katikati ya Mji wa Morogoro.
Kwa upande wake Bi Faraja Mwakabeta Mama mzazi wa mchezaji huyo alipotakiwa kutoa ushauri kwa Kijana wake alijibu.
“Siwezi kusema chochote mpaka nipate ruhusa kwa Mwanangu leo wanamechi na KMC baada ya mchezo nitazungumza naye namba yangu unayo utanipigia kesho akitoa ruhusa tutazungumza ”alisema Mama huyo Mluguru wa Morogoro.
Chaajabu baada ya nusu saa majira ya saa 7 na dakika 1 Dickson Job alimpigia simu Mwandishi wa habari hizi na maongezi yao yalikuwa hivi.
Job. Habari za Morogoro.
Mwandishi, Nzuri habari za huko.
Job, Njema nani kakupa ruhusa ya kwenda kuwahoji wazazi wangu?
Mwandishi. Kwa Mwandishi yoyote anapoona habari haitaji kuhusa ya mtu yoyote kwenda kufanya kazi yake.
Nimesoma habari zako kwenye moja ya gazeti ukihusishwa kuhitajika na Simba hivyo walipoishiwa waandishi wenzangu mimi nimejiongeza nimeenda mbele zaidi kuzungumza na wazazi wako juu ya tetesi hizo.
Pili mbona ulivyokuwa Moro Kids tulikuwa tunakupiga picha na kuandika habari zako zilizochangia mafaniko yako hukufoka?
kwa sasa uko Yanga ndio unatoa kauli hizo kumbuka wewe kwa sasa ni star kina unachofanya ni habari.
Baada ya kuambiwa hivyo Job amekaa kimya kisha amekata simu.
Mara nyingi Mwandishi wa Mtandao huu anapozungumza na wachezaji kutoka Morogoro iwe kwa simu au Live wanampa ushirikiano.
Wachezaji hao ni Nickson Kibabage, Kibwana Shomari na Kipa Abuutwarib Msheli{Yanga].
Shomari Kapombe Mzamiru Yassini na Ladack Chasambi[Simba]
Wengine ni Offen Chikolla [Tabora United] Shiza Kichuya[JKT Tanzania] Zuberi Dabi Mashujaa] Salum Kihimbwa{Chuji] Fountaine Gate na Ismail Mgunda Maarufu Suma[ As Vita ya DR Congo]
No comments:
Post a Comment