Baadhi ya makaburi ya nduigu zetu Wahindi yakiwandani ya fensi kando kando ya barabara ya Forest Mafuta ya Mtume Mwamposa yakiwa kwenye kichupa hicho kidogo chenye mfuniko mweupe.Mama huyu anayedaiwa kuwanga akiendelea kugaragara chini baada ya kuondolewa katikati ya barabara
HABARI KALI YA KITAA.
MWANAMKE
ANASWA USIKU MNENE MAKABURI YA WAHINDI AKIDAIWA KUWANGA.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Kama kawaida
kipengele pendwa cha habari kali ya kitaa kinaendele leo ljumaa.kabla ya
kuendele nitoe mrejesho wa habari iliyopita.
Niliahidi
kuendelea kumtafuta yule bibi aliyedaiwa kumfanyia vitu vya ajabu marehemu
mumewake,juhuzi hizo zimegonga mwamba kila nikimpigia simu kupitia no yake ya tigo
mwisho 10 haipatikani.
Majirani
wanadai ameludi kijijini kwao Mgeta na wengine wanadai amekwenda Dar kwa watoto
zake.
Majirani hao
wamesema huenda huko kamua kukata mawasiliano kwa kubadili namba ya simu.
TUENDELEA NA STORI MPYA
MWANAMKE
Mmoja ambaye hajafahamika mara moja anayekadiliwa kuwa na Umri kati ya Miaka 35
mpaka 40, anadaiwa kukutwa usiku Mnene eneo la Makaburi ya Watanzania wenye
asiri ya lndia ‘Wahindi’yaliyopo ‘ushuani’ eneo wanaloishi Mabosi na matajiri Forest Mkoani hapa akiwa uchi wa mnyama
akidaiwa kufanya vitendo vya
kishirikina’kuwanga.
Akizungumza
na Mtandao huu Shuhuda wa tukio hilo
Nickson Mkilanya’Nick Fado’ alisema.
”Juzi majira
ya saa 6 usiku nikiwa ndani ya gari langu nilipofika eneo la Makaburi ya
Wahindi nilikuta foreni kubwa ya magari na Pikipiki niliposogea jirani
nimeshuhudia huyu Mama akiwa uchi wa Mnyama akisota kwenye lami jirani na geti
la makaburi ya wahindi ”alisema Mkilanya na kuongeza
“Inaonekana amenasa kwenye makaburi hayo ya ndugu zetu
Wahindi, kwa sababu alikuwa katikatia ya barabara madereva wameogopa kumgonga
wameishi kummulika na taa baada ya foreni kuwa kuwa kubwa mtu mmoja kajitolea kumpa nguo na kumuondoa
eneo la barabara kuruhusu gari zipite.
Alivyovaa nguo
nikampiga hizi picha za Video na Mnato ambazo nimekurushia kwenye Whatsapp yako,
nasikia alfajiri alitoweka kimiujiza”alimalizia kusema Mkilanya ambaye ni
Mwenyekiti wa chama cha Waandishi wa
habari Mkoa wa Morogoro.
Baada ya
kupewa ‘Tip’ hiyo Mwandishi wa habari hizi aliingia mzigo akatinga eneo la
tukio na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo ambao walikuwa na haya ya kusema.
“ Taarifa
hizo hatuna si unajua huku Forest ni uzunguni nyumba nyingi zina mageti muda
wote mchana na usiku watu wako ndani ya
mageti yao yanayotokea huko nje hatuyajui”walisema wananchi hao.
Mtandao huu
alimtafuta Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo wa Old Dar es salaam Mzee Asanali.
”Binafsi
sina taarifa za tukio hilo ninachoweza kusema ni kwamba taarifa hizi
nitazipeleka BMK pia nitamfahamisha polisi Kata aimalishe ulizi kwenye makaburi
yale ambayo tumeyazungushia uzio yakjo
ndani ya geti”alimalizia kusema Mwenyekiti huyo ambaye ni pia ni Muhindi.
Chaajabu
baada ya habari hii kukamilika kwa maana ya kuzungunza na mashuhuda pamoja na
Uongozi wa Serikali ya Mtaa Mwandishi alipofungua picha za Mama huyo Whatsapp
hakuziona.
Hivyo jana
mchana imemradhimu kumpigia Mkilanya na
kumjuza taarifa hizo, ‘Big Bos’ huyo wa Waandishi wa habari mkoa aliangua kicheko kisha akatuma tena picha hizo
za Mnato na Video, muda huu kabla ya kuzifungua
Mwanahabari huyo aliamua kujipaka
mafuta ya Mtume Mwamposa mwili mzima na kuzifungua picha hizo safari hii
zilifunguka fasta.
Clips Video
inayomuonyesha Mama huyo akisota barabara nimeshindwa kuirusha kwa kuzingatia
maadili kwa sababu alikuwa akifanya hivyo akiwa uchi wa mnyama.
lfahamike
Mtaa wa Old Dar unaanzia eneo la daraja la Shan sinema Kitope Road kando kando
ya barabara ya zamani ya Dar es
salaam,ndani ya Mtaa huo kuna kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Morogoro, Uwanja wa Jamhuri, Hospital
ya Rufaa ya Mkoa, Chuo cha VETA, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi za Posta mkoa,
Hazina Mkoa C.A.G Mkoa, NSSF Mkoa. Madini Mkoa, Maktaba ya Mkoa Msikiti Mkuu wa
Wahindi ‘Jamatini’na Shule ya Sekondari ya Morogoro.