Na Dustan Shekidele,Morogoro.
MTANDAO Pendwa wa Shekidele unawatakia heri ya Mwaka Mpya wadau wote wa Mtandao huu,pia unamuomba Mwenyezi Mungu awaponye haraka wagonjwa wote waliolazwa mahospital na wale wa majumbani wakipigania uhai wao.
Hali kadharika Mtandao huu unatoa pole kwa ndugu na jamaa waliopoteza ndugu zao mwaka uliopita, huku tukimuomba Mwenyezi Mungu awasamehe makosa yao Marehemu wote na wawake pale wanapostahiri kwa jinsi walivyoishi hapa duniani.
Ama baada ya salama hizo za Mwaka mpya tuingie kwenye kipengele chetu pendwa cha stori kali ya Kitaa, tunaanza Mwaka na stori kali kutoka Juu ya Milima ya Uluguru mitaa ya Morning Site Kata ya Mlimani Manispaa ya Morogoro.
Kwa mujibu wa wenyeji wa Mkoa wa Morogoro wanadai juu ya Mlima huo uliopo jirani na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro unavivutio vingi baadhi ya vivutio hivyo ni Ndege wenye rangi za bendera ya Taifa la Tanzania na eneo ambalo muda wote wa giza na Jua lina kuwa na kivuli Januari mpaka Desemba.
Kufuatia hali hilo wenyeji wameamua kuliita eneo hilo Morning Site kwa sababu muda wote muonekana wake ni kama majira ya asubuhi.
Usafiri rahisi wa kufika juu ya kilele cha Mlima huo ni Pikipiki, Mwandishi wa Mtandao huu alipiga gia mmoja ya pikikiki zake akapanda juu ya Mlima huo kushuhudia vivutio hivyo.
Baada ya kutua juu ya kilele na Chopa yake ya Boda boda Mwanahabari huyo aliwashuhudia wenyeji wakilima mazao mbali mbali kando kando ya Mito iliyopo juu ya Mlima huo.
Miongoni mwa mazao hao ni pamoja na Matunda ya Kauberi yanayopendwa zaidi na wazungu, pichani Mwanahabari huyo akikagua zao hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mh Mussa Kilakala akizungumza na kituo kimoja la Redio Mkoani Morogoro hivi karibuni alisema Mlima huo unavivutio Vingi wakiwemo Ndege wenye rangi za bendera ya Taifa ambao hawapatikani popote zaidi eneo hilo.
Tukutane wiki ijayo kwa kwa habari kali ya kitaa
No comments:
Post a Comment