.....Vulugu hilo likiendelea
Kiongozi wa waamuzi wilaya ya Morogoro Mwarabu Mumba kulia akijadiliana jambo na Mratibu wa michuano hiyo Amir Salum
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
KAMWE Derby ya Ndondo Cup kati ya mahasimu wakubwa wenye mashabiki wengi mkoani Morogoro, Black Viba na Black People haijawa kuwa nyepesi hata kidogo.
Hali hiyo imedhihirika juzikati kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ndondo Cup uliopigwa uwanja wa Saba saba .
CHANZO CHA VULUGU.
Dakika ya 57 Mwandishi wa Mtandao huu aliyekuwa nyuma ya gori la Kaskazini Mwa Uwanja wa Saba saba akiwa na kamera yake kubwa yenye uwezo wa kupiga picha uwamba wa mita 300.
Alishuhudia kundi la mashabiki wakimshushia kichapo mshika kibendera namba moja aliyefahamika kwa jila na Juma,kufuatia hali hiyo mshikakibendera huyo aliamua kutoka uwanjani kwa lengo la kuoka maisha.
Baada ya gemu hiyo kuvunjika vulugu hizo ziliendelea kila timu ikihitaji kupewa ushindi hali hiyo ilipelekea Polisi kuingia uwanjani na kutuliza vulugu hizo.
Ili kujua hatima ya mchezo huo ambao hadi unavunjika timu hizo zilikuwa sare ya bao 1-1 Mwandishi wa habari hizi alimtafuta mratibu wa michuano hiyo Bw Amir Salum,alipotakiwa kuelezea hatima ya mchezo huo alikuwa na haya ya kusema.
“ Kwa sasa siwezi kusema lolote kwa sababu unahitajika umakini wa hali ya juu wa kutoa maamuzi ya haki, kweli mchezo umevunjika baada ya mashabiki kumvamia Mshikakibendera, wale mashabiki hatujui ni watimu gani, hivyo tuwe na subra hivi karibuni nitaketi na kamati yangu ya mashindano na tutatoa maamuzi ya haki kwa timu zote mbili”alisema Salumu ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama cha Soka Wilaya ya Morogoro.
No comments:
Post a Comment