Nickson Kibabahe mwenye jezi nyeupe akiwa na baadhi ya wachezaji aliocheza nao utotoni........Kibabage jezi no 3 akikiwasha kwenye gemu ya timu Kibabage na timu ya Mti Mchungu Fc........Kibabage akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu mara baada ya gemu hiyo kutamatika.....Kibabage akiendelea kukiwasha kwenye gemu hiyo Kibabage bakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu zote mbili
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
HABARI ya Mujini kwa sasa ni ‘Gusa AchiaTwende Kwao’ Mwendo wa 5G.
Beki
kilaka wa Yanga Nickson Kibabage Mkazi wa Mawezi Kata ya Kiwanja cha
Ndege Morogoro, ameipeleka Gusa Achia nyumbani kwao Morogoro.
Mara
baada ya Mabingwa hao wa kihistoria ‘Wazee wa Supu’ wenye Maskani yao
Makutano ya Mitaa ya Twiga na Jagwani Kariako, kuichapa Fountain Gate
mabao 5-0 Juzi uwanja wa KMC Mwenge Dar.
Kibabage
aliyekuwa sehemu ya gemu hiyo alipiga gia gari yake na kuja nyumbani
kwao Morogoro siku iliyofuata yaani Jana Kibabe aliwakusanya wachezaji
aliocheza nao Mtaani kwao, Moro Kids na Mtibwa Sugar wakaunda timu
waliyoipa jina Timu Kibabage.
Baada ya Kibabage
kuunda timu hiyo wakacheza gemu ya kirafiki na timu ya Mti Mchungu Fc
uwanja wa Shule ya Msingi Saba saba Kata ya Kiwanja cha Ndege.
Kwenye gemu hiyo iliyojaza umati mkubwa wawatu waliofika kumshuhudi kijana wa Mtaa kwao anayefanya vizuri Yanga.
Timu Kibabage walipoke kichapo cha bao 2-0 toka kwa Mti mchungu Fc
inayoungwa na wachezaji wengi wa timu ya Moro Stars inayoshiriki Ligi
daraja la Nne Wilaya ya Morogoro.
Mara kadhaa kibabage akipogusa Mpira mashabiki hao wake kwa waume waliipa ‘Gusa Achia Twende Kwao’.
Gemu ilipotamatika Mwandishi wa habari hizi alizungumza na Kibabage alipotakiwa kueleza dhumuni la mchezo huo alisema.
”Nimechi
ya kirafiki nimekusanya wachezaji niliocheza hao utotoni hapa Mtaani
kwangu na wale niliocheza nao Moro Kids na Mtibwa Sugar”alisema
Alipoulizwa
Yanga wanajiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabigwa Afrika dhidi ya TP
Mazembe utakaopigwa Januari 4 Uwanja wa Mkapa Dar iweje yeye yuko
Morogoro?
Alijibu. “ Mara baada ya gemu ya jana na
Fountain Gate kutamatika tulipewa ruhusa ya siku 2 kwa maana ya Leo na
kesho tunahitajika kulipoti kambini Januari Mosi, hivyo baada ya kupewa
off jana hiyo hiyo nimekuja nyumbani Morogoro na leo nimeandaa
mchezo”alimalizia kusema Kibabage.
Baadhi ya Mastaa
walioshuhudiwa na Mwandishi wa habari hizi wakiitumikia timu ya Kibabage
ni pamoja na Omari Manga Maarufu ‘Adebayo’ anayeitumikia Mtibwa B na
George Chota anayeitumikia timu ya Mtibwa ya wakubwa inayoongoza Ligi
daraja la kwanza kwenye mchezo wa juzi Mtibwa iliibuka na ushindi wa bao
3-0 huku Chota akifunga bao la 2.
No comments:
Post a Comment