Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Jumanne ya Leo kipengele chetu Pendwa cha Fagio la Mtaa kinaendelea kwa habari ya Mama Lishe kupika Wali bila uwepo wa matandu ya Juu kwa lengo la kujiongezea kipato huku baadhi ya wateja wake wengi wao wakiwa madereva wa boda boda wakikerwa na jambo hilo.
Fagio la Mtaa likiwa Mitaani kusaka habari kali ya wiki lilikatiza kwenye vijiwe vya boda boda maeneo Mji Mpya na kushuhudia baadhi ya boda boda hao wakiwajadili Mama Lishe hao wanaopika wali bila Matandu.
Walipoulizwa kwa nini wanakerwa na hali hio boda boda hao walisema.
”Unajua maisha yetu ni unga unga Mwana hizi Pikipiki ni za makataba tajiri anataka kipande cha elfu 10 kila Day, utafute pesa ya mafuta kila siku, kama hiyo tumepanga wenye nyumba wanataka kodi zao sambamba na michango ya bill za Maji na Umeme.
Sasa bila kumeck huwezi kutoboa hivyo katika hali hiyo ya kubana matumizi mara nyingi tunakwenda kwa Mama Mtilie kula spea kwa maana ya matandu ya juu au ule ukoko wa chini ambao tunauziwa kwa bei poa na kipimo chake ni kikubwa”walisema boda boda hao na kuongeza kudadavua.
“Hayo matandu ukiyamwagia chuzi la nyama yanarainika unakula vizuri tu siku inapita, sasa kitendo cha baadhi ya Mama Lishe kupika wali bila Spea wanatukosea”walisema wafukuza upepo hao.
Kufuatia hali hiyo Mwandishi wa habari hizi alitinga kwa Mmoja wa Mama Lishe hao maeneo ya Mji Mpya na kushuhudia akipika Wali bila uwepo wa matandu ya juu.
Akizungumza na na Fagio la Mtaa,Mama Lishe huyo aliyejitambulisha kwa Jina la Mama Mussa alisema.
“ Ni kweli kama unavyoona ndio namaliza kupika Wali na hauna matatu juu tunafanya hivi kwa lengo la kujiongezea kipato, mchele bei mbaya sasa chini kukiwa na ukoko na juu kikiwa na matunda kipimo kimapungua kwa sababu ukoko na matandu yanachukua mchele mwingi”alisema Mama Lishe huyo na kuongeza.
Kama unavyoona ninawafanyakazi natakiwa kuwalipa, sisi wanawake tuna mikopo na michezo ya kupea pesa tunasomesha watoto sasa kama usipokuwa mbunifu unakula kwako”alisema Mama Mussa pichani nayekaanga dagaa.
Alipoulizwa kuhusu malalamiko ya baadhi ya wateja kukosa matandu Mama Lishe huyo alijibu.
Wao wanakula matandu kwa lengo la Kumeck na Mimi pia napika bila matandu kwa lengo hilo hilo la Kumeck hivyo ngoma Droo ‘ubaya ubwela”alisema Mama Mussa na kuangua kicheko.
Alioulizwa anaika je mpaka matandu yanakosekana mama Mussa alijibu.
“ Hatuvunikii na mkaa juu watu wa pwani tunaita kupalilia, badala yake kuna kitu tunaweka juu na wali unawiva vizuri kabisa na hakuna tandu hata moja kama unavyoona huo wali hapo ndio umeiba nimeutoa jikoni sasa hivi sijapakua hata sahani moja”alisema Mama Lishe huyo.
Banda la Mama Mussa lipo Mtaa wa Makaburi ‘A’ Kata ya Mji Mpya jirani na Kituo cha Polisi Kata, Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata, Zahanati ya Kata ya Mji Mpya na Stend ya daladala ya Kaloleni jijiga Mji Mpya.
Uchunguzi wa awari uliofanywa na Mwandishi wa habari hizi umebaini baadhi ya watumishi wa taasisi hizo za serikali wanaagiza chakula kwa Mama Mussa.
Hii ni kufuatia chakula kitamu kinachopikwa na Mama huyo anayezingatia pia usafi kwenye mapishi yake.
No comments:
Post a Comment