Mfungaji wa mabao hayo D Maria akizungumza na Mtandao huu.
Mh Kihanga akimkabidhi kombe Nahodha wa Kilo Net Carles Mrichi.
Mh Kihanga akiwa katika picha ya pamoja na mabingwa hao wa mkoa.
Na Dustan Shekidele Morogoro.
Subra ni lbada na Mvumilivu hula mbivu.misomo hiyo imetimia jana kwa timu ya Kilo Net Fc kutwaa Ubingwa wa Ligi daraja la Tatu Mkoa wa Morogoro, baada ya kukosa kwa misimu miwili ikifungwa kwenye faibali.
Kilo Net Fc inayomilikiwa na Taasisi ya kukuza na kuibua Vipaji ya Kilombero Soccer Net Academy yenye maskani yake lfakara Wilaya ya Kilombero, imenyakua ubingwa huo kwa mara ya kwanza baada ya kuwafunga majirani zao Usalama Fc kutoka Wilaya ya Ulanga.
Katika mchezo huo wa fainali uliopigwa uwanja wa Jamahuri Manispaa ya Morogoro Kilo Net waliwanyuka Wanausalama hao kwa chuma 2-0.
Huku mbao yote yakifungwa na Haroun Tumbagani Maarufu D. Maria bao la kwanza akifunga dakika ya 10 kipindi cha kwanza na la pili alilifunga dakika 88 ya kipindi cha pili na kupeleka majonzi kwa wanausalama hao.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Morogoro’MRFA’ Jimmy Lengwe alisema timu 8 kutoka Wilaya zote 7 za mkoa wa Morogoro zilishiriki fainali hizo zilizoanza kutimua vumbi Novemba 29 uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro na kutamatika jana Desemba 5 uwanja wa Jamhuri.
” Awari Ligi hii ilichezwa kwa kanda 4 wilaya zote za Mkoa wa Morogoro kila kanda ikitoa timu 2 ambazo ni Usalama kutoka Wilaya ya Ulanga.Challenge Fc na Cypilian Fc kutoka Wilaya ya Malinyi, Wallers Fc, Mang’ura Fc na Kilo Net kutoka Wilaya ya Kilombero nyingine ni Mafisa United na Morogoro Tanzanite Soccer Academy’MOTASO’ kutoka Wilaya ya Morogoro Mjini yenye muunganiko na Wilaya ya Morogoro Vijijini”alisema Lengwe.
Kwa upande wake Mgeni rasmi wa fainali hiyo Mstahiki Meya wa Mji wa Morogoro Mh Pascal Kihanga ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mazimbu na Mwenyekiti wa chama cha Soka Mkoa wa Morogoro.
Kwenye hotuba yake aliwataka mabingwa hao kuanza mapema maandalizi wa michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa na kuuwakilisha vyema mkoa wa Morogoro.
Mtandao huu umekusanya matukio mengi kwenye fainali hiyo hivyo usicheze mbali na mtandao huu.
No comments:
Post a Comment