Mwili ukiwasili nyumbani kwa marehemu
......ukiwa kwenye gari tayari kw akuelekea Mmbete
umati wawatu uliofurika jana kushiriki mazishi ya Mpendwa wetu Rhumba Boy.
Rhumba Boy enzi za Uhai wake akicharaza Tumba za band ya Waluguru Og.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
WANANCHI Mkoa Morogoro wamejitokeza kwa wingi jana kumzika Msanii Maarufu wa Muziki wa Dansi nchini Kondo Seleman Rhumba Maarufu ‘Rhumba Boy’.
Marehemu Rhumba ambaye miaka ya 90 alifanikiwa kutwaa ubingwa wa kusakata Disko Mkoa wa Morogoro, alifariki dunia juzi Octobar 1 na kuzikwa jana kwenye makaburi ya familia yao yaliyopo eneo la Mmbeta Keleka Juu ya Milima ya Uluguru.
Baada ya kuachana na kusakata Disko hayati Rhumba aliyejaliwa vipaji vingi na Mwenyezi Mungu alitimkia kwenye muziki wa Dansi na kuzitumikia band mbali mbali za Mkoani Morogoro kama vile Waluguru Original, Maisha Mapya Misic Band na Mikumi Sound, band aliyoitumikia hadi umauti unamkuta.
Kwenye band hizo Rhumba alikuwa akitunga nyimbo na kuziimba yeye mwenyewe miongoni mwa nyimbo hizo ni wimbo wa Ua jekundu. Kama hiyo haitoshi Rhumba Boy akikuwa na uwezo wa kupiga Drum huku anaimba, kupigaTumba, Gitaa la Bass na kucheza shoo’ kudensi’
Kwa sasa band ya Mikumi Sound inayotamba na kibao chake cha ‘Mama Mkwe Kisa gani’inayomilikiwa na Mgos Josse Kigenda imehamia Turiani Wilaya Mvomero.
Mwandishi wa habari hizi aliyekuwepo msibani nyumbani kwa marehemu Mitaa ya Mafisa [4 Ways] jirani na daraja la Kichangani alishuhudia mastaa kibao wakijitokeza kumzika Staa mwenzao.
Kama kawaida Mpiga Picha wa Mtandao huu alifanikiwa kuwachapa mapicha Mastaa hao ambapo picha zao zitaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
WASIFU WA MAREHEMU.
Kwa bahati mbaya wasifu wa marehemu haukusomwa kwa sababu za ufinyu wa muda, baada ya mwili kuwasili majira ya saa 6 mchana ukitokea Moswari uliswaliwa hapo hapo nyumbani kisha kuingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea Mmbeta kumpunzisha kwenye nyumba yake ya Milele.
Ili kukamilisha habari hii kwa kupata historia ya Marehemu,Mtandao huu ulizungumza na Aziza selema Kondo ambaye ni Mtoto mkubwa wa marehemu.
Alipotakiwa kuelezea wafisu wa mpendwa baba yake alisema.
”Kwa niaba ya familia tunakushukuru SANA Shekidele kwa sapoti yako kwenye msiba wa Mpendwa baba yetu.
Wasifu wa baba.
Alizaliwa miaka 50 iliyopita na alisoma shule ya Msingi Mwembesongo, alipomaliza elimu ya Msingi alijihusisha na sanaa ya kucheza Disko hadi umauti unamkuta alikuwa Mwanamuziki wa band ya Mikumi Sound..
Marehemu baba ameacha watoto 6 na wajukuu 11” alisema Aziza.
Siku chache kabla ya kuanza kuugua Rhumba Boy alikutana na Mwandishi wa Mtandao huu maeneo ya Mji Mpya akasema.
"Shekidele ngoja niwaandae watoto zangu 6 na wajukuu zangu 11 nikuite unipige nao picha ya pamoja kama kumbuku" tamanio lake hilo halikutimia hadi mauti inamkuta
No comments:
Post a Comment