Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, October 2, 2024

MWANAMUZIKI MAARUFU MORO AFARIKI DUNIA


                                          Rhumba Boy enzi za uhai wake

Na Dunstan Shekidele, Morogoro.
Mwanamuziki Maarufu Mkoani Morogoro aliyekuwa akiitumikia Band ya Mikumi Sound’Wana tekenya’ Kondo Seleman Rhumba’Almaarufu Rhumba Boy’amefariki dunia alfajiri ya leo hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro alipolazwa kwa wiki kadhaa akipatiwa matibabu.
Taarifa za kifo cha Mwanamuziki huyo ambaye pia ni Densa aliyewahi kutwaa ubingwa wa kusakata Disko Mkoa wa Morogoro miaka ya 90, zilianza kutapakaa jana lakini baadae ilibainika kwamba Rhumba Boya hajafariki duniani angawa alikuwa akuendelea kuupigani uhai wake
kwa kupumulia mashine chumba cha wagonjwa mahututi’I.C.U’ Mapema asubuhi ya leo taarifa hizo ziliibuka tena kwa kasi kubwa hali iliyopelekea Mwandishi wa habari hizi kumpigia simu Aziza Seleman Kondo ambaye ni mtoto mkubwa wa Marehemu
na kuthibitisha kifo cha Mzee wake huyo.
” Ni kweli shekidele mzee amefariki leo alfajiri na msiba uko hapa nyumbani Mafisa jirani na daraja la kuelekea Kichanganga tumapanga kuzika kesho saa 7
mchana”alisema Aziza Maarufu Mama Ally.
Enzi za uhai wake mara baada ya kuacha kusakata Disko Rhumba Boy akijiunga na muziki wa dansi akizitumikka Band mbali mbali akipiga Drum, Kucheza na kucheza.
Hadi umauti unamkuta Rhumba Boy alikuwa akiitumika Band ya Mikumi Sound’Wana Tekenya’akitamba na wimbo wake Ua Jekundu alioutunga kuimba huku akipiga Drum. Panapo Majaliwa ya Mwenyezi Mungu
Mwandishi wa Mtandao huu atashiriki mazishi hayo na kukusanya matukio yote yatakajiri kwenye msiba huo.
“Bwana ametoa na Bwana ametwa jina lake lihimidiwe.
Tangulia Kamanda Tutaonana Baadae”

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...