Mwenyekiti wa matawi ya Yanga Mkoa wa Morogoro Issa Kitukwa Maarufu ‘Issa Chabala’ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Serikali ya Mtaa wa Fumilwa B.Kata ya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro.
Anayefuata ni Mbaraka Mlanzi ‘Ubuge’ Agent wa mabasi ya Al- Saed Stend ya Dodoma Awari Mlanzi alipangiwa kituo cha Chalinze kabla ya Uongozi wa Al- Sead yenye makao yake Mkuu Msamvu mkoani Morogoro.
Kulia kwa Mlanzi ni Bure Mtagwa Kipa wa zamani wa Kagera, Sugar, Sigara, Reli, Moro United na timu ya Taifa ya Tanzania’ Taifa Stars’
Wa Mwisho ni Baba lbram Mkaa. Mzee huyo Mwanye lbra Mkaa anaitumikia timu ya Moro Kids.
Killer Boy
Bob Tiger akiweka pozi matata baada ya kuona kamera za Mtandao huu zikimlulika
Mpiga Drums Maarufu mkola wa Morogoro Calvin katilingi Maarufu sayota sebondo.akiwa msibani.
Sebondo wakati akiitumika band ya Waluguru alikuwa akipokezana kupiga Drum na hayati Rhumba Boy.
Kwa sasa Sebondo anacharaza Drums za Band ya Maisha Mapya.
Babu Kichuya
Mmiliki wa Band ya Waluguru Original Deogratius Alphonce Maarufu ‘Killer Boy’ akipokea dua mara baada ya mwili wa hayati Rhumba Boy kuswaliwa.
Picha no 2 Killer na wasanii wenzake wakiwasili Msibani hapo
Mzee lbrahim Mangwende ‘Maarufku Babu Kichuya’ambaye ni babu wa mchezaji wa JKT Tanzania Shiza Ramadhan Kichuya naye alishiriki kwenye Msiba wa Rhumba Boy.
Dj Sweet Cofe[kushoto]akizungunza na Mwandishi wa Mtandao huu, kulia ni Mpiga Kinanda Maarufu Mkoa wa Morogoro Mussa Mishe Mishe ‘Jeshi la Mtu Mmoja’.
lfahamika Sweet Cofe na Dj John Peter miaka ya 90 ndio walikuwa Ma Dj kwenye ukumbi wa shimoni wa Morogoro Hotel wakidondosha mawe kwenye mashindano ya kusaka Ubingwa wa kusakata Disko Mkoa wa Morogoro.
Akizungumza na Mtandao huu Msibani hapo Sweet Cofe alisema akiwa Dj Mwaka 92 Rhumba Boy alifanikiwa kunyakua Ubingwa wa Mkoa akiwabwaga wapinzani wake wakubwa Super Ngedere na Bob Tiger.
Mwanamuzi Jumanne Maaeufu J4 mwenye flana ya mistari ya njano akiwa na wasanii wenzake wakiendesha harambee ya kumchangia mwenzao.Maneno Ngedere ‘Maarufu Super Ngedele’kulia akiwa na Lucas Wales Maarufu Bob Tiger. Wawili hao ndio walikuwa wapinzani wakubwa wa Hayati Rhumba Boy kwenye mashindano ya Disko Mkoa wa Morogoro Super Ngedele ndio anayeongoza kutwaa ubingwa huo mara nyingi akifuatiwia na Bob Tiger huku Rhumba Boy akishika nafasi ya tatu.
Bob Tiger ambaye toka miaka ya 90 alitimkia nchini Uingereza anakoishi mpaka sasa akiwa na familia yake. lkumbukwe miaka hiyo ya 90 kwenye mashindano ya Disko mrembo mmoja wa kizungu raia wa Uingereza aliyekuwa nchini kwa shughuri Maarumu TX alivutiwa na uchezaji wa Bob Tiger na kuvutiwa na uchezaji wa Tiger na kujikuta akizama kwenye wimbi la Mahaba. Baada ya mkataba wake wa kufanya kazi hapa nchini na kutakiwa kurejea kwa Uingereza aliamua kuondoka na Tiger. Rast Man
Kwa sasa Tiger amerejea hapa nchini kwa mapunzika huku mkewe na wanae wakisalia huko Uingereza.
Picha zote na Dustan Shekidele,Morogoro.
No comments:
Post a Comment