Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, October 17, 2024

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu
.....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya
...Miili ya marehemu ingiinizwa kwenye majeneza tayari kwa kuelekea msikittini
                              .......Safari ya kuelekea msikitini


                      Marehemu Sebuge enzi za uhai wake

 

     Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

INASIGITISHA SANA. Muuza Magazeti Maarufu mkoani Morogoro  Sebuge Mohamed, anadaiwa kujinyonga hadi kufa, muda mfupi baada ya kutoka kwenye kikao cha  familia ya Mazishi ya Mpendwa dada yake Marehemu Mwahamisi Kaliati aliyefariki dunia Octobar 12.

Tukio hilo la kujinyonga limetokea usiku wa Octobar 13 nyumbani kwa Marehemu Sebuge Mtaa wa Ngoma B Kata ya Mji Mpya mkoani hapa,  muda mfupi baada ya Sebuge kutoka kwenye kikao hicho kilichofanyika  majira ya jioni nyumbani kwa marehemu Mwanahamisi  Mtaa wa River Side Kata ya Mwembesongo.

Mara baada ya Mwandishi wa habari hizi kushiriki mazishi ya marehemu hao   waliosaliwa na kuzikwa siku moja Makaburi ya Kolla  Octobar 14,

Siku iliyofuata Octobar 15 Mwanahabari huyo aliingia mzigoni kwa kuwahoji watu mbali mbali wakiwemo wanafamilia na viongozi wa serikali ya Mtaa.

Mtandao huu ulifanikiwa kuzungumza na Bi.  Pili Sebuge ambaye ni Mama wa marehemu wote wawiwli waliozima ghafra kama mshumaa.

Alipotakiwa kueleza vifo hivyo  Bi’Mkubwa huyo alisema.

” Inauma sana Mwanangu Mwahamisi ambaye ni Mtoto wa dada yangu aliyeniachia ziwa alifariki kifo cha kawaida,siku iliyofuata tumeketi kikao cha familia cha kupanga mazishi.

  Sebuge ambaye ni Mtoto wangu wa kwanza  kumzaa aliketi hapo ulipokaa wewe akiongoza kikao hicho tukaamua Mwahamisi tumzike Ochotar 14.

Sebuge akatapanga wachinga Kaburi la dada’ke  wapishi na watu watakao kwenda kwa Abood kuomba basi”alisema Mama huyo na kuongeza.

Baada ya kikao kutamatika Mwanangu alimuacha mkewe hapa akatuaga kaenda kulala kwake.

Pale kwake anaishi na mwanae pamoja na Mpwa wake mtoto wa huyo Marehemu Mwanahamisi na kila siku alfajiri Mwanangu Sebuge huwaamsha hao wanae na kwenda kuswari ile swala ya saa 11alfajiri.

Kwa sababu watoto walishazoe kuswali swala hiyo baada ya kuona hawakuamshwa wakahisi labda baba yao ametangulia msikitini, wakaende msikitini walipomaliza kuswali hawakumuoba.

Ndipo waliporejea nyumbani walipoingia  chumbani chake wamemkuta Mwanangu ananing’inia juu ya paa amejinyonga”amesema Bi Mkubwa huyo na kuangua kilio na kushindwa kuendelea na mahojiano.  

Kwa pande wake Bi Aziza Omary ambaye ni Mke wa Marehemu alipohojiwa alisema.”Baba yetu wa familia ameondoka ameniachia malezi ya watoto wengu kinachoniuma zaidi  mtoto wetu Mohamed siku 6 mbele anatakiwa kujiunga chuo cha Afya baada ya kuhitimu kidato cha 6”alisema Mjane huyo na marehemu na kuangua kilio.

Akitoa mawaidha kabla ya marehemu wote wawili kwenda kuswaliwa Msikiti wa Mwembesongo, Shehe Maulid Baggo alisema.” Baada ya ndugu yetu kujinyonga watu walisema mengi kuhusiana na uhalali wa kumswalia au kutomswalia.

Kwa msikiti wetu wa Mwembesongo tunaamini anayetoa huku ni mwenyezi Mungu pekee na si mwanadamu hivyo tubebe maiti zote mbili tukaziswalie pale msikitini kisha tukazike”alisema Shehe Baggo na kupokea zawadi ya makofi  kutoka kwa Umati wawatu walifurika msibani hapo mtaa wa River Side .

Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Daniel Matonya alithibitisha Mwananchi wake kujinyonga ndani ya mtaa wake.

Alipoulizwa kama anajua chanzo cha mwananchi wake huyo kuchukua maamuzi hayo magumu ya kujitoa uhai, mwenyekiti huyo alisema.

“ Baada ya kupokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa wananchi alfajiri ya siku ya tukio awari nilimpigia Mh Diwani Emmy Kiula, baadae nikampiga simu Polisi walifika wakaushusha mwili kisha wakaupekua mwili wa marehemu kama kuna ujumbe wowote amkeandika.

Kweli kwenye mfuko wake walikuta barua ndefu polisi wakamwita Mtoto wa marehemu wakamuuliza huu ni mwandiko wa baba yako? Mohamed baada ya kuangalia ile barua kasema ni mwandiko wa baba yake.

Kilichoandikiwa hata mimi mwenyekiti sikuambiwa hivyo sijui chanzo cha kifo ninachoweza kuthibitisha kwako ni kwamba marehemu ameacha jumbe”amesema Mwenyekiti huyo.

Mtandao huu unatoa pole kwa familia, Mungu azidi kuwatia nguvu kwenye kipindi hichi kigumu mnachopitia cha kuondokewa na wapendwa wetu .

                

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...